Ripoti mpya yabainisha matukio ya mateso na mauwaji Burundi
5 Novemba 2021Katika ripoti hii ya sasa ya Shirika la Haki za Binaadamu laki za Binadamu la Burundi ambalo limekuwa likifutatilia hali ya masuala ya kiutu nchini Burundi, kunaelezwa kwamba maafisa kutoka usalama wa taifa hilo pamoja na polisi watuhumiwa kwa kutesa, kuuwa na kupoteza watu katika mazingira ya utatanishi.
Ripoti hiyo inasema wanaofanya vitendo hivyo wapo huru kabisa kuwafuatilia wale wanaoshukuwa kuwa wapinzani na kitisho kwao na kuwafanya chchote watakacho.
Mambo yamekuwa mabaya zaidi tangu katikati ya mwaka 2021.
Ripoti inasema tangu katikati ya mweka huu wa 2021, uelekeo wa Burundi katika suala la haki za binaadamu umegeuka kuwa mbaya zaidi. Baada ya mfululizo wa mashambulizi ya wenye kujihami kwa silaha katika kipindi cha Aprili na Septemba 2021, maafisa wa serikali wamewatuhumu wapinzani kwa kushirikiana na makundi yenye kujihami kwa silaha na kuwateka au kuwakamata wengi wao.
Hali inatajwa kuendelea kuwa hivyo, pamoja na kutolewa kwa lugha ya kidiplomasia ya amani na usalama, likiwemo hakikisho la Ndayishimiyewe mwenyewe kwamba hali ya upatikanaji haki katika taifa lake imeboreshwa. Ndayishimiye alichaguliwa kuwa rais wa Burundi Mei, 2020 ikiwa baada ya kifo cha aliyekuwa rais wa taifa hilo Pierre Nkurunziza.
Wito kwa rais Ndayishimiye kuachana na mwenenendo wa Nkurunziza.
Makundi ya haki za binadamu yamekuwa yakimtaka kutofuata nyendo za ukandamizaji za mtangulizi wake. Hata hivyo baada ya shutuma zilizomo katika ripoti hii ya sasa shirika la habari la AP lilifanya jitihada zilizogonga mwamba za kutaka kuzungumza na msemaji wa serikali Prosper Ntahorwamiye.
Akizunguma katika Hadhara Kuu ya Umoja wa Mataifa, Ndayishimiye alisema serikali yake ina lenga katika kulinda haki za binadamu, kuheshimu kanuni za kidemokrasia, uhuru wa kujieleza na wa kutoa maoni. Lakini baadhi ya watu wameonesha kutokubaliana na hilo.
Mwanasiasa wa upinzani wa Burundi, ambae kwa sasa anaishi uhamishoni, mjini Brussels Ubelgiji Aime Magera anasema hotuba hiyo haina ukweli na kudai kwamba wapinzani wanauwawa, wanateswa na kukamatwa kiholela na kufungwa na vyombo vya usalama vya serikali.
Ripoti nyingine inasema miili ya watu zaidi ya 60 imekutwa katika eneo la mto Rusizi.
Ripoti ya Shirika la Haki za Binadamu la Burundi inasema vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu vimeongezeka katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni, ambapo tangu Julai kumeripotiwa visa vya watu takribani 20 kutoweshwa. Mara nyingi baadhi wanawekwa kizuizini katika makao makuu ya idara ya upelezi ya taifa mjini Bujumbura na kudaiwa kuteswa.
Ripoti inasema baadgi ya hao wapo wanaoachiwa huru lakini wapo ambao hawajasikika tena hadi sasa. Mashirika mengine yametoa ripoti kama hiyo. Kundi la waandishi wa habari la Burundi SOS Medias Burundi, ambalo linafanya kazi ndani ya taifa hilo hivi karibuni lilisema tanguJanuari limeweza kuhesabu miili ya watu zaidi ya 60 katika eneo la mto Rusizi ambao unayatenganisha maitafa ya Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Chanzo: AP