1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Macky Sall ampongeza Bassirou Faye kwa ushindi Senegal

26 Machi 2024

Kiongozi wa upinzani asiye na umaarufu mkubwa nchini Senegal Bassirou Diomaye Faye mwenye umri wa miaka 44, ametangazwa kuwa rais mpya wa Senegal.

https://p.dw.com/p/4e7kP
Rais Mteule wa Senegal Bassirou Diomaye Faye
Rais Mteule wa Senegal Bassirou Diomaye FayePicha: Luc Gnago/REUTERS

Faye ameshinda uchaguzi mkuu nchini humo, wiki mbili tu baada ya kuachiwa huru kutoka jela ili ashiriki uchaguzi huo. Huku ikiwa matokeo rasmi yakiwa bado hayajatangazwa, waziri mkuu wa zamani aliyekuwa anaungwa mkono na Rais Macky Sall, amekiri kushindwa kutokana na matokeo ya awali.

Soma pia: Faye aahidi kuitawala Senegal kwa unyenyekevu na uwazi

Rais Sall pia amempongeza Faye akimtaja kwamba yeye ndiye mshindi. Ushindi wa Faye unaonyesha hali ya kukata tamaa ya vijana ambao hawana ajira na ushindi huo unaonyesha pia hofu iliyopo kuhusiana na masuala ya uongozi katika taifa hilo la Afrika Magharibi.

Katika hotubya yake ya kwnaza kama rais mteule, Faye ameahidi kufungua ukurasa mpya kufuatia miezi kadhaa ya kamata kamata ya kisiasa na machafuko.