1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Hamid Karzai kujadiliana na Musharraf

26 Desemba 2007

---

https://p.dw.com/p/CgPm

ISLAMABAD

Rais Hamid Karzai wa Afghanstan yuko Pakistan kwa ajili ya kukutana kwa mazungumzo na rais Musharaf kwa lengo la kushirikiana katika kupambana dhidi ya wanamgambo wa Taliban na Al-Qaeda kwenye eneo la mpaka baina ya nchi hizo mbili.

Rais Karzai pia anatarajiwa kutumia mkutano huo kuzungumzia uhusiano wa kibiashara kati ya Pakistan na nchi yake.

Aidha rais Karzai amepangiwa pia kukutana na waziri mkuu wa muda anayeshikilia nafasi hiyo hadi utakapofanyika uchaguzi wa bunge mwezi ujao.