1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Rais Emmanuel Macron kulihutubia taifa Jumatano

21 Machi 2023

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anatarajiwa kulihutubia taifa kesho Jumatano siku mbili baada ya serikali yake kunusurika kupigiwa kura ya kutokuwa na imani nayo, kufuatia mageuzi ya mfumo wa pensheni

https://p.dw.com/p/4OyTs
Frankreich Rentenrefrom l Misstrauensvotum gegen Macron
Picha: Michel Euler/Pool via REUTERS

Hotuba yake itarushwa na vituo mbali mbali  vya televisheni nchini humo kesho mchana. Watu chungunzima walikamatwa kote nchini humo kufuatia maandamano yaliyozuka  saa chache baada ya serikali kunusurika kupigiwa kura ya kutokuwa na imani nayo bungeni jana Jumatatu.

Hatua ya bunge imempa afueni rais Macron na serikali yake kuendeleza mageuzi yake ya kuongeza umri wa kustaafu kutoka miaka 62 mpaka 64.

Soma pia: Serikali ya Ufaransa yanusurika chupuchupu kura za kutokuwa na imani bungeni 

Wabunge wa Upinzani wameapa kushinikiza kuzuia hatua hiyo na vyama vya wafanyakazi vinajiadaa kuchukua hatua ya maandamano ya nchi nzima mnamo siku ya alhamisi.