1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Qatar:Operesheni za Israel zazorotesha mazungumzo ya amani

14 Mei 2024

Qatar ambayo ni msuluhishi katika mazungumzo ya kutafuta amani kati ya Israel na kundi la wanamgambo la Hamas,leo imesema operesheni za kijeshi zinazofanywa na Israel katika Rafah zimeyarudisha nyuma mazungumzo hayo.

https://p.dw.com/p/4fqaa
Uharibifu baada ya mashambulizi ya Israel katika kambi ya wakimbizi ya Jabaliya
Moshi unafuka kufuatia eneo la mashambulizi ya Israel katika kambi ya wakimbizi ya Jabaliya, kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, Mei 13, 2024.Picha: Abdul Rahman Salama/Xinhua/IMAGO

Waziri mkuu wa Qatar Mohammed bin Abdulrahman Al-Thani ameuambia mkutano wa kiuchumi unaofanyika nchini humo, kwamba katika kipindi cha wiki chache zilizopita, wameshuhudia hatua zikipigwa lakini kwa bahati mbaya mambo hayakwenda vizuri na hivi sasa wamefikia katika hatua ya kuelekea kwenye mkwamo. Qatar imekuwa ikishirikiana na Misri na Marekani kwa miezi kusimamia mazungumzo ya upatanishi kati ya pande hizo mbili. Israel imeendelea kulishambulia kundi la Hamaskatika mji wa Rafah ,licha ya kauli za kuonywa na Marekani dhidi ya kufanya mashambulizi makubwa katika mji huo wa Kusini mwa Ukanda wa Gaza unaokaliwa na maelfu ya Wapalestina.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW