1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lützerath: Wanaharakati wa mazingira wapambana na polisi

Zainab Aziz
10 Januari 2023

Polisi nchini Ujerumani imesema imeanza kuviondoa vizuizi vilivyowekwa na wanaharakati wa hali ya hewa kwenye kijiji cha Lüzerath waandamnaji hao wanapinga kupanuliwa mgodi wa makaa ya mawe.

https://p.dw.com/p/4LyVa
Deutschland Klimaaktivistinnen blockieren die Räumung von Lützerath
Picha: Michael Probst/AP Photo/picture alliance

Mamia ya wanaharakati wa hali ya hewa wamekuwa wakikimiliki kijiji cha Lüzerath, magharibi mwa Ujerumani, wakijaribu kuilazimisha mamlaka kusitisha upanuzi wa mgodi mkubwa wa makaa ya mawe unaomilikiwa na kampuni ya nishati ya Ujerumani RWE.

Takriban wanaharakati 200 wamejikita kwenye kijiji hicho kilichotelekezwa, huku polisi wakijiandaa zaidi kuingia mahala hapo ili kuwaondoa waandamanaji katika zoezi linalotarajiwa kuanza siku chache zijazo. Kulingana na polisi, operesheni kubwa ya kuwaondoa waandamanaji itaanza kesho siku ya Jumatano na kwamba inaweza kuchukua muda wa wiki nzima.

Polisi wamwondoa mwanaharakati wa mazingira katika kijiji cha Lützerath
Polisi wamwondoa mwanaharakati wa mazingira katika kijiji cha LützerathPicha: Michael Probst/AP Photo/picture alliance

Kijiji cha Lützerath kimepangiwa kubomolewa ili kutoa nafasi kwa upanuzi wa mgodi huo utakaofikia ukubwa wa kilomita  mraba 35 na unatarajiwa kuwa na uwezo wa kuzalisha tani milioni 25 kwa mwaka za makaa ya mawe aina ya "lignite” yanayotoka kwenye mwamba laini na kufahamika kama makaa ya kahawia.

Mnamo siku ya Jumapili, maandamano hayo yalihudhuriwa na maelfu ya watu waliokitembelea kijiji hicho cha Lüzerath ambapo pia walipanga kujumuika kwenye mkesha wakati ambapo kulikuwa na tamasha la muziki wa bendi ya Kijerumani ya AnnenMayKantereit lakini baadae makabiliano na polisi yalizuka. 

Kampuni kubwa ya nishati ya RWE inanuia kuendelea na zoezi la kupanuza mradi wake katika Kijiji cha Lützerath. Wakazi wa eneo hilo kwa muda mrefu sasa wameondoka kutoka kwenye eneo hilo, lakini wanaharakati wamevamia majengo kadhaakatika eneo hilo wa miezi kadhaa na idadi yao imeongezeka katika wiki za hivi karibuni.

Kushoto: Mwanaharakati mashuhuri wa mazingira Luisa Neubauer.
Kushoto: Mwanaharakati mashuhuri wa mazingira Luisa Neubauer.Picha: David Young/picture alliance/dpa

Mamia ya wanaharakati walishikana mikono na kuunda minyororo ya binadamu na hivyo kutengeneza kizuizi kwa kukaa chini, huku baadhi ya waandamanaji wakijichimba karibu nusu mita ardhini. Waanfdmanaji hao wameungwa mkono na baadhi ya wanasiasa kama Janine Wissler, kiongozi wa chama cha mrengo mkali wa kushoto cha Die Linke, pamoja na wanaharakati mashuhuri wa mazingira kama Luisa Neubauer.

Vyanzo: DPA/AP