1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Gregor Gysi

Gregor Gysi ni mwanasiasa wa Ujerumani kupitia chama cha mrengo wa kushoto cha Die Linke. Alikuwa msemaji mkuu wa upinzani katika bunge (Bundestag) kufutia uchaguzi mkuu wa mwaka 2013.

Gysi, aliezaliwa 1948 anachukuliwa kuwa mmoja wa wazunguzaji bora zaidi nchini Ujerumani. Baada ya kunaguka kwa utawala wa GDR mwaka 1989 mwanasheria huyo wa zamani wa Ujerumani Masahriki aliongoza chama cha Umoja wa Kisoshalisti nchini Ujerumani SED, ambacho baadae kilijibadili na kuwa chama cha Demokrasia ya Kisoshalisti PDS, ambacho baadae tena kiliungana na chama cha WASG cha Ujerumani Magharibi na kuunda chama cha sasa cha mrengo wa kushoto cha Die Linke. Gysi anakanusha madai kuwa alikuwa mtoa habari katika wizara ya usalama wa taifa ya Ujerumani Mashariki, Inayofahamika zaidi kama Stasi. Mwaka 2004 alinusurika operesheni ya ubongo na mshtuko wa moyo. Ukurasa huu ni mkusanyiko wa maudhui za DW kumhusu Gysi

Onesha makala zaidi