Inspekta Mkuu wa Polisi ya Tanzania Simon Sirro amesema uchunguzi ambao wameufanya umeonyesha kwamba gari lililotumiwa kumteka nyara mfanyabiashara Mo Dewji lilitoka nchi jirani. Hayo ameyasema jijini Dar es Salaam, akiviarifu vyombo vya habari kuhusu maendeleo yaliyopatikana katika uchunguzi juu ya utekaji nyara wa Dewji uliofanyika zaidi ya wiki moja iliyopita. Papo kwa Papo 19.10.2018