1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi sita wajeruhiwa kwenye vurugu katika mji wa The Hague

Sudi Mnette
18 Februari 2024

Polisi 6 wamejeruhiwa huku watu 13 wakitiwa mbaroni baada ya kutoka vurugu kwenye mji wa The Hague nchini Uholanzi.

https://p.dw.com/p/4cYCl
Mahakama ya Kimataifa ya Haki | Kesi ya mauaji ya kimbari ya Israel | Tangazo kuhusu maombi ya dharura | polisi
Mwonekano wa Jumba la Amani, ambalo lina Mahakama ya Kimataifa ya Haki, au Mahakama ya Kimataifa, huko The Hague, Uholanzi, Ijumaa, Januari 26, 2024.Picha: Patrick Post/AP Photo/picture alliance

Vurugu hizo kati ya wafuasi na wapinzani wa serikali ya Eritrea zimesababisha pia uharibifu mkubwa wa mali. Polisi imesema maafisa wake na wahudumu wa huduma ya dharura walipigwa mawe na fataki wakati makundi hayo mawili yanayopingana yalipopambana huku ikisema watu 13 wametiwa mbaroni kufuatia mkasa huo. Magari mawili ya polisi na basi moja yameteketea kabisa, huku magari mengine yakiharibiwa vibaya. Eneo la mkutano lililoandaliwa na kundi linaloiunga mkono serikaya Eritrea pia limeharibiwa. Polisi wa kutuliza ghasia walilazimika kutumia gesi ya kutoa machozi ili kutuliza ghasia. Meyawa mji wa The Hague, Jan van Zanen, amelaani ghasia hizo na ameamrisha hali ya hatari katika eneo la tukio.