1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washukiwa wa mauaji ya Fleurs wakamatwa Afrika Kusini

10 Aprili 2024

Polisi nchini Afrika Kusini imesema leo kuwa imewakamata washukiwa sita wa mauaji ya mwanasoka Luke Fleurs aliyekuwa anachezea kilabu maarufu ya Kaizer Chiefs mjini Johannesburg.

https://p.dw.com/p/4edXU
Afrika Kusini
Polisi wa Afrika KusiniPicha: Jon Hrusa/dpa/picture alliance

Msemaji wa polisi Mavela Masondo, amesema washukiwa hao wamekamatwa kwa madai ya utekaji nyara na mauwaji.

Maafisa nchini humo wanasema kuwa wiki iliyopita, Fleurs alikuwa anasubiri kuhudumiwa katika kituo kimoja cha kujaza gari mafuta wakati alipovamiwa na wanaume wawili waliomtaka atoke nje ya gari lake kabla ya kumpiga risasi na kutoroka na gari hilo.

Masondo amesema washukiwa hao walikamatwa mjini Johannesburg siku mbili baada ya maafisa wa uchunguzi kupata gari lake. 

Maafisa hao wa upelelezi wanaamini kuwa washukiwa hao ni sehemu ya mtandao wa uhalifu unaohusika na wizi wa utekaji nyara wa magari mjini Johannesburg katika mkoa wa Gauteng.