Pik Botha wajihi wa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini afariki | Matukio ya Afrika | DW | 12.10.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Pik Botha wajihi wa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini afariki

Pik Botha waziri wa mwisho wa mambo ya nje wa utawala wa ubaguzi wa rangi na mtengano wa Afrika Kusini-Apartheid amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 86. Alikuwa mwanasiasa shupavu kabla ya kukiri mageuzi hayaepukiki.

Botha amefariki dunia leo alfajiri akiwa nyumbani kwake baada ya kuuguwa kwa muda mfupi, amesema mwanawe wa kiume Roelf Botha mbele ya maripota wa kituo cha matangazo cha Afrika Kusini eNCA news.

Kimataifa Pik Botha alikuwa mwakilishi bayana wa mfumo wa ubaguzi wa rangi na mtengano-apartheid, katika wakati ambao utawala huo ulikuwa ukizongwa na malalamiko na vikwazo vya kimataifa, malalamiko yaliyomalizikia kwa kuchaguliwa Nelson Mandela kuwa rais wa kwanza mweusi mwaka 1994.

Alitetea hatua za serikali yake kila mahala ingawa alitambua baadae umuhimu wa mageuzi. Aliwashangaza walimwengu na hasa rais wa Afrika Kusini wakati ule P.W. Botha aliposema mwaka 1986 Afrika Kusini inaweza siku moja kuongozwa na mtu mweusi.

Rais wa mwisho wa utawala wa kibaguzi wa Afrika Kusini Frederik de Klerk akipeana mkonon na Nelson Mandela mwaka 1993 baada ya kutunukiwa nishani ya uhuru ya Philadelphia na kushangiriwa na rais wa wakati ule Bill Clinton miongoni mwa wengine

Rais wa mwisho wa utawala wa kibaguzi wa Afrika Kusini Frederik de Klerk akipeana mkonon na Nelson Mandela mwaka 1993 baada ya kutunukiwa nishani ya uhuru ya Philadelphia na kushangiriwa na rais wa wakati ule Bill Clinton miongoni mwa wengine

"Mustakbali wa Afrika Kusini utaakuwa mwema waafrika na wazungu wakiungana" anasema Pik Botha

"Tunabidi tufanikiwe. Ulimwengu unataka tufanikiwe. Katika wakati ambapo enzi za ubaguzi wa rangi na mtengano apartheid zinatoweka kitakuwa kiroja kikubwa na balaa kama wa-Afrika Kusini watashindwa kujongokeana na kukubaliana kusonga mbele na kuigeuza nchi yao iwe ya kidemokrasi, kama tulivyostahiki kuwa na kupata sifa ambazo nchi yetu inazostahiki."

Pik Botha ambae hatokani na ukoo mmoja na rais wa zamani wa Afrika Kusini P.W. Botha, aliteuliwa kuwa waziri wa maadini na nishati katika serikali ya Nelson Mandela na kusema mwaka 2000 angependelea kujiunga na chama cha African National Congress ANC-chama tawala kilichoendesha mapambano kwa miongo kadhaa dhidi ya utawala wa wazungu wachache.

Nelson Mandela na Cyril Ramaphosa mwaka 2005

Nelson Mandela na Cyril Ramaphosa mwaka 2005

Pik Botha amefurahishwa na kukabidhiwa Cyril Ramaphosa hatamu za uongozi wa Afrika Kusini

Lakini kuanzia wakati ule Pik Botha alikuwa tayari ameanza kujitenga na siasa. Matamshi yake ya mwisho aliyoyatoa miaka ya hivi karibuni yalihusiana na kashfa iliyomkaba rais wa zamani Jacob Zuma aliyejiuzulu february iliyopita."Botha alifurahi sana aliposikia Cyril Ramaphosa amekabidhiwa nafasib ya Zuma, alisikia  Pik Botha akisema. Itafaa kusema Pik Botha aliyekuwa waziri wa mambo ya nchi za nje kati ya mwaka 1977 hadi mfumo wa aparthheid ulipokoma mwaka 1994, alihusika na mazungumzo mwishoni mwa miaka ya 80 yaliyopelekea Namibia kupata uhuru .

 

Mwandishi:Hamidou Oumilkheir/AP/Reuters

Mhariri :  Mohammed Abdul-Rahman

Matangazo

IJUE DW

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com