Papa Leo XIV atoa ujumbe wa matumaini kwa Walebanon
1 Desemba 2025
Matangazo
Wito wa Papa Leo unawalenga vijana ambao imani yao imedidimia katika taifa ambalo limezongwa na migogoro.
Maelfu ya Walebnon walijitokeza barabarani kumpokea Papa Leo licha ya mvua.
Baada ya kuwasili Lebanon akitokea Uturuki katika ziara yake ya kwanza kimataifa kama Papa, Leo aliomba katika kaburi la Mtakatifu Charbel Makhlouf, kiongozi wa kidini Lebanon aliyeheshimiwa na Wakristo na vilevile Waislamu.
Papa Leo anatarajiwa kukutana na viongozi wa kanisa la Katoliki nchini humo wakiwemo maaskofu na watawa kisha ataongoza mkutano wa Pamoja unaozileta dini mbalimbali pamoja na viongozi wa Kikristo na Kiislamu wa Lebanon mjini Beirut.