JamiiAngola
Papa Leo XIV aongoza misa kubwa nchini Angola
20 Aprili 2026
Matangazo
Papa Leo alitembelea pia eneo takatifu la Mama Muxima pembezoni mwa Mto Kwanza na alifanya ibada katika hekalu la Kikatoliki lililokuwa kitovu cha biashara ya watumwa wa Kiafrika wakati wa utawala wa wakoloni wa Ureno huku akikukumbuka "huzuni na mateso makubwa" ambayo Waangola walivumilia kwa karne nyingi.
Angola ni kituo cha tatu katika ziara ya Papa Leo barani Afrika . Baada ya Angola, anatazamiwa kuelekea Guinea ya Ikweta atakapohitimisha ziara yake ya siku 10 itakayokamilika Aprili 23, 2026.