Olmert kwa Merkel | Matukio ya Kisiasa | DW | 12.02.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Olmert kwa Merkel

Waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert akutana na Kanzela Merkel wa Ujerumani mjini Berlin.

Kanzela Angela Merkel wa Ujerumani amemhakikishia waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert kumuungamkono barabara katika mgogoro wa Mashariki ya kati.Alisema kwamba, Ujerumani inaungamkono jitihada za suluhisho la dola 2-Israel na palestina.A,kaongeza kusema wakati wa mkutano wake na Olmert katika afisi yake mjini Berlin, kwamba muda unapita .Nae waziri mkuu wa israel akasisitiza kwamba hujuma zinazofanywa kutoka ardhi za wapalestina dhidi ya Israel zikome.

Baada ya mazungumzo yake na kanzela Angela Merkel wa Ujerumani mjini Berlin,waziri mkuu ehud Olmert wa Israel ameitisha jumuiya ya kimataifa kuimarisha juhudi zake katika mvutano na Iran juu ya mradi wake wa kinuklia.Akasema uwezekano wote lazima uzingatiwe ili kuutatua mzozo huo.Olmert ana yakini kwamba uongozi nchini Iran unaoendesha mpango wa siri wa kuunda silaha za kinuklia.

Kanzela Angela merkel kwa upande wake amezungumzia hali ngumu iliopo katika utaratibu wa kusaka amani Mashariki ya kati.Alisema wakati wa mazungumzo unapita na kwamba Ujerumani yaungamkono ufumbuzi chini ya msingi wa dola mbili-ile ya Israel na ya wapalestina.

"Kwetu sisi ni muhimu sana kwamba pamoja na jukumu la kihistoria la kudhamini kuwapo kwa dola la Susrael,usuhuba wetu wa pande mbili uwekwe kwenye jukwaa linalotupa macho hali ya usoni na kujenga mahusiano sio tu katika sekta ya kiuchumi bali pia ya taftishi za kisayansi na hasa kuwakutanisha watu wa pande hizi mbili."

Ujerumani inapanga kuungwamkono juhudi zake na Israel lakini pia na washirika wake wa kipalestina.Zinaungwa mkono juhudi pia za waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair kama mjumbe wa lile kundi la pande 4 kuhusu mgogoro wa Mashariki ya kati. Kanzela Merkel akasema kuna maswali mengi ambayo hayajapata bado majibu na pia kumebakia swali la kuizuwia Iran isirutubishe madini ya uranium-jambo ambalo bado halikufanyika.

Akasema wamefuata mkakati wa ncha mbili-kwa upande mmoja kuiwekea Iran vikwazo ikiwa haitaitikia masharti ya shirika la nguvu za atommiki ulimwenguni (IAEO) na kwa upande mwengine tumeinyoshea mkono wa ushirikiano ikiitikia madai ya jamii ya kimataifa-alisema Kanzela Angela Merkel.

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com