1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obama apata ushindi Washington,Luisiana na Nebraska

10 Februari 2008

Bado lakini kinyang'anyiro kiko mbali kumtambua nani zaidi

https://p.dw.com/p/D58z

WASHINGTON

Katika kinyang'anyiro cha kugombea uteuzi wa vyama wa mgombea urais nchini Marekani kwa upande wa chama cha Demokratic Barack Obama amenyakua ushindi katika majimbo ya Washington na Nebraska dhidi ya mpinzani wake Hillary Clinton.Katika uchaguzi huo ambao unafanyika kwenye majimbo manne Obama tayari amejipatia asilimia 67 katika jimbo la Washington wakati Clinton akizoa asilimia 32 pekee.Ingawa matokeo haya yanamuweka mahala pazuri Barack Obama lakini bado kuna kura za wajumbe 78 pamoja na wajumbe maalum ambao wanajulikana kama Super Delegates ambazo zitaamua hatma ya nani atakuwa mgombea wa wademokrat katika uchaguzi wa rais wa mwezi Novemba.

Katika chama cha Republican Mike Huckabee ameshinda jimbo la Kansas lakini bado yuko mbali kumfikia mpinzani wake John McCain.Matokeo ya upande wa chama cha Demokratic yanaonyesha ni jinsi gani seneta wa jimbo la Illinois Barack Obama anavyozidi kupata umaarufu tangu kufanyika kwa chaguzi za kile kilichoitwa Super Tuesday.