Nigeria, Burkina Faso nani zaidi Fainali? | Michezo | DW | 07.02.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Nigeria, Burkina Faso nani zaidi Fainali?

Nigeria na Burkina Faso zitakutana katika fainali ya mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika katika uwanja wa Soccer City siku ya Jumapili, baada ya timu zote kupata ushindi mkubwa katika hatua ya nusu fainali Jumatano.

Mali ikuchana na Nigeria katika mchezo wa nusu fainali katika uwanja wa Moses Madiba mjini Durban siku ya Jumatano

Mali ikuchana na Nigeria katika mchezo wa nusu fainali katika uwanja wa Moses Madiba mjini Durban siku ya Jumatano

Nigeria iliigagadua Mali magoli 4 - 1 mjini Durban, ikionyesha mchezo maridhawa kabisaa kuliko ulioonyeshwa na timu yoyote katika mashinda hayo, kwa kufunga magoli matatu kabla ya mapumziko. Burkina Faso, ambao walikuwa hawahesabiwi kabisaa wakati wanaanza mashindano hayo waliilazimisha Ghana sare ya goli 1 -1 baada ya muda wa nyongeza kabla ya kupata ushinda wa magoli 3 -2 katika mikwaju ya penati, katika nusu fainali nyingine iliyochezwa katika uwanja wa Sandy Mbombela mjini Nelspruit.

Mubarak Wakaso wa Ghana akifunga goli la kwanza dhidi ya Burkina Faso mikwaju ya penati Jumatano.

Mubarak Wakaso wa Ghana akifunga goli la kwanza dhidi ya Burkina Faso mikwaju ya penati Jumatano.

Jambo pekee lisilojema kwa timu ya Burkina Faso maarufu kama Stallions, ni kupigwa marufuku kutocheza fainali za Jumapili, kwa winga wao hatari Jonathan Pitroipa, aliyeonyeshwa kadi ya pili ya njano kwa kujiangusha dakika tatu kabla ya kumalizika kwa muda wa nyongeza. Hata hivyo Kocha Paul Put alisema baadaye kuwa timu itawasilisha pingamizi mara moja dhidi ya uamuzi huo wa mwamuzi kutoka Tunisia, Slim Jedidi.

Nigeria yasaka taji la kwanza baada ya miaka 19

Hii itakuwa fainali ya saba kwa Nigeria wanaosaka taji lao la kwanza katika kipindi cha miaka 19, na ya kwanza kwa Burkina Faso, ambao wameonyesha kiwango bora kuliko walichokionyesha mwaka 1998 walipofikia hatua ya nusu fainali nchini kwao. Walionyesha pia uwezo wa kutochoka haraka walipolaazimishwa kucheza muda wa nyongeza siku ya Jumapili kabla ya kuishinda Togo kwa goli 1 - 0 katika mchezo wa robo fainali.

Kocha wa Nigeria Stephen Keshi sasa ana nafasi ya kuwa mtu wa pili katika historia ya miaka 56 ya mashindano hayo kushinda taji kama kocha na mchezaji akifuata nyayo za Mahmoud El Gohary wa Misri aliyeshinda taji mwaka 1959 kama mchezaji, na mwaka 1998 kama kocha nchini Burkina Faso. Kocha Stephen hivi sasa anaonekana kama ndiye mtu muhimu zaidi katika mchezo wa soka wa Afrika na mashabiki wa Nigeria wanaamini timu yao iliyojaa vijana wadogo itafanya mambo makubwa zaidi.

[36815568] Africa Cup of Nations 2013 Ejike Uzoenyi (kushoto) wa Nigeria, akigombania mpira na Adama Tamboura wa Mali wakati wa mchezo wa nusu fainali mjini Durban siku ya Jumatano.

Ejike Uzoenyi (kushoto) wa Nigeria, akigombania mpira na Adama Tamboura wa Mali wakati wa mchezo wa nusu fainali mjini Durban siku ya Jumatano.

Utendaji wa timu ya Burkina Faso unatoa nafasi ya ukombozi kwa Kocha Put ambaye alipigwa marufuku kutojihusisha na mpira maisha katika nchi yake ya Ubelgji baada ya kushiriki sakata la kupanga matokeo mwaka 2007. Michezo yote miwili ya nusu fanali ilikuwa ya kusisimua kufuatia masimulizi mawili tofauti kabisaa.

Ghana sasa itakabiliana na Mali katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu mjini Port Elizabeth siku ya Jumamosi wakati Nigeria na Burkina Faso zikijiandaa kwa kilele cha mashindano hayo mbele ya mashabiki elfu 90 siku ya Jumapili.

Mwandishi: Iddi Ismail Ssessanga/rtre
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

DW inapendekeza