1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AFCON 2013: Macho yote kwa Cape Verde

2 Februari 2013

Wakati Afrika kusini itaungwa mkono na mashabiki wake katika mpambano leo(02.02.2013)wa robo fainali ya kombe la mataifa ya Afrika dhidi ya Mali, kurunzi ya kimataifa itamulika vijana kutoka visiwa vya Cape Verde.

https://p.dw.com/p/17Wuy
Football - 2013 Africa Cup of Nations - Qualified Teams - Cape Verde. Cape Verde Team Group URN:15454270
Kikosi cha timu ya taifa ya Cape VerdePicha: picture-alliance/empics

Wakaazi hao wa visiwani wanapambana na vigogo wa soka barani Afrika Ghana katika mchezo mwingine leo wa robo fainali mwanzoni mwa awamu ya mtoano katika fainali hizi za 29 mwaka huu.

Cape Verde, ikiwa na idadi ya wakaazi wapatao zaidi ya nusu milioni tu na kundi dogo la wachezaji ambao wanaweza kuitwa kucheza timu ya taifa , wamewaacha mashabiki wa soka midomo wazi na kunyakua nafasi miongoni mwa timu nane bora katika bara la Afrika , katika mara yao ya kwanza kushiriki katika mashindano haya makubwa katika bara la Afrika.

Titel: Lúcio Antunes - Trainer der Fußball-Nationalmannschaft der Kapverden Ort: Praia, Cabo Verde Fotograf: Nélio dos Santos Datum: 20.10.2012 Beschreibung: Lúcio Antunes, der als Trainer der Fußball-Nationalmannschaft der Kapverden, es zum ersten Mal geschafft hat, dass sich die Kapverden für eine Afrika-Fußball-Meisterschaft qualifiziert haben. Die Inselrepublik wird in Südafrika 2013 zum ersten Mal an einem Africa Cup of Nations teilnehmen.
Kocha wa Cape Verde Lucio AntunesPicha: DW/Nélio dos Santos

Ushindi wa kushangaza dhidi ya Angola katika mchezo wao wa mwisho katika kinyang'anyiro cha makundi , kufuatia sare mara mbili, umewafanya wakaazi hao wa visiwani kuwa kionjo maridadi kwa wapenzi wa soka duniani kote.

Cape Verde ghafla imetoka kutoka timu ngeni katika mashindano haya na kuepuka kuaibishwa na kuwa timu ambayo inaamini kuwa inaweza kufikia nusu fainali.

Cape Verde kunyakua kombe?

"Hii ni timu yenye kujiamini na tumezidi sasa kujiamini tangu mashindano haya yaanze. Tuna uwezo, " amesema kocha Lucio Antunes.

Ghana wana mchezaji Mubarak Wakaso, ambaye amefunga bao pekee wakati walipoishinda Cape Verde katika mchezo wa kirafiki nchini Ureno mwezi Novemba, ambaye anarejea uwanjani mjini Port Elizabeth baada ya kukaa nje kutokana na kadi nyekundu.

Mpambano huo unafuatiwa na mpambano baina ya wenyeji wa mashindano Afrika kusini maarufu kama Bafana Bafana mjini Durban dhidi ya Mali , timu ambayo imemaliza ikiwa yatatu katika kinyang'anyiro cha mwaka jana.

DURBAN, SOUTH AFRICA - JANUARY 27: May Mahlangu of South Africa celebrates his goal with team mates during the 2013 African Cup of Nations match between Morocco and South Africa at Moses Mahbida Stadium on January 27, 2013 in Durban, South Africa. (Photo by Steve Haag/Getty Images)
Bafana Bafana wakishangiria baoPicha: Getty Images

"Kucheza na wenyeji wa mashindano na mashabiki wao wakiwa nyuma yao ni hadhi kubwa na changamoto kubwa , tunashauku na tunalisubiri kwa hamu pambano hili, amesema kocha Patrice Carteron.

Bundesliga

Na katika bundesliga, Nils Petersen alipachika mabao mawili katika mpambano wa duru ya 20 katika bundesliga na kuipa Werder Bremen ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Hannover 96, ikiwa ni ushindi wa kwanza wa Bremen katika mwaka huu jana Ijumaa.

Bremen walitengeneza nafasi kadhaa za kufunga kabla ya Petersen hatimaye kuvunja ukame wa magoli kwa timu hiyo katika dakika ya 85, wakati Eljero Elia alipowatoka walinzi wawili wa Hannover na kummegea pande mfungaji.

Fußball Bundesliga, 20. Spieltag, Werder Bremen - Hannover 96 am 01.02.2013 im Weser Stadion in Bremen. Werders Nils Petersen jubelt über sein Tor zum 2:0. Foto: Carmen Jaspersen dpa - (Achtung! Hinweis zur Bildnutzung! Die DFL erlaubt die Weiterverwertung von maximal 15 Fotos (keine Sequenzbilder und keine Fotostrecken) während des Spiels (einschließlich Halbzeit) aus dem Stadion und/oder vom Spiel im Internet und in Online-Medien. Uneingeschränkt gestattet ist die Weiterleitung digitalisierter Aufnahmen bereits während des Spiels ausschließlich zur internen redaktionellen Bearbeitung (z.B. via Bilddatenbanken). +++(c) dpa - Bildfunk+++
Petersen wa Bremen akishangiria moja ya mabao yake mawili dhidi ya HannoverPicha: picture alliance / dpa

Bremen ilitengeneza nafasi 32 za kufunga ikilinganishwa na sita za Hannover . Kocha wa Bremen Thomas Schaaf amesema kuwa, ingekuwa maafa makubwa iwapo tusingetumia nafasi tulizozipata. Ushindi huo unaiinua Bremen hadi nafasi ya 11, point moja nyuma ya Hannover, kabla ya michezo mingine hii leo na kesho.

Leo (02.02.2013) Fortuna Dusseldorf inaikaribisha VFB Stuttgat, Mainz ina kibarua na viongozi wa ligi hiyo Bayern Munich, Hoffenheim inaikaribisha nyumbani Freiburg, wakati Schalke 04 iko nyumbani ikiwakaribisha Greuther Fuerth. VFL Wolfsburg ina miadi na FC Augsburg, wakati Eintracht Frankfurt inasafiri hadi mjini Hamburg kupambana na klabu ya mjini humo.

Borussia Dortmund's Felipe Santana (C) celebrates his goal with Mario Goetze (L) and Kevin Grosskreutz during their German Bundesliga first division soccer match against Werder Bremen in Bremen January 19, 2013. REUTERS/Wolfgang Rattay (GERMANY - Tags: SPORT SOCCER) DFL RULES TO LIMIT THE ONLINE USAGE DURING MATCH TIME TO 15 PICTURES PER GAME. IMAGE SEQUENCES TO SIMULATE VIDEO IS NOT ALLOWED AT ANY TIME. FOR FURTHER QUERIES PLEASE CONTACT DFL DIRECTLY AT + 49 69 650050
mabingwa watetezi Borussia Dortmund watapambana na LeverkusenPicha: Reuters

Kesho Jumapili (03.02.2013) itakuwa ni zamu ya mabingwa watetezi Borussia Dortmund ambayo itakuwa na mpambano wa kuamua nani hasa anashika nafasi ya pili wiki hii kati yake na Bayer Leverkusen. Leverkusen inashikilia nafasi ya pili hadi sasa na Dortmund inashikilia nafasi ya tatu, timu hizo zinapishana kwa point moja. Nuremberg ina miadi na Borussia Moenchengladbach.

Liverpool na Manchester City

Wakati huo huo Meneja wa Manchester City Roberto Mancini amewaonya wachezaji wake kuwa Liverpool ina uwezo wa kutoa pigo jingine katika matumaini yao ya kuwania taji la msimu huu katika mpambano wao kesho Jumapili(03.02. 2013).

Mabingwa hao watetezi wa Premier League wamepoteza nafasi ya kutoa mbinyo kwa viongozi wa ligi ya msimu huu Manchester United wakati walipolazimishwa sare ya bila kufungana na QPR katikati ya wiki na wanaweza kurudi nyuma hadi kupishana na Manchester United kwa points kumi wakati watakapokumbana na Liverpool kesho.

epa03379076 Manchester City's Edin Dzeko (L) celebrates his goal against Queens Park Rangers with teammates Carlos Tevez (C) and Samir Nasri during the English Premier League soccer match between Manchester City and QPR at the Etihad Stadium in Manchester, Britain, 01 September 2012. EPA/LINDSEY PARNABY DataCo terms and conditions apply http//www.epa.eu/downloads/DataCo-TCs.pdf +++(c) dpa - Bildfunk+++
Wachezaji wa Manchester CityPicha: picture-alliance/dpa

Iwapo United itaishinda Fulham leo , utetezi wa City wa taji lake utakuwa katika hatari kubwa na Mancini anatambua fika kuwa Liverpool ina vipaji ambavyo vinaweza kuongeza matatizo kwa timu yake.

Mancini pia ana matumaini kuwa miezi ya Februari na Machi ambayo United itakuwa na michezo mingi na migumu ambapo itakumbana na Real Madrid katika kinyang'anyiro cha Champions League cha timu 16 zilizobaki, huenda ikapoteza points katika ligi ya nyumbani.

Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre / afpe

Mhariri : Iddi Ssessanga