Nhlanhla Nene: Mikataba kuhusu Gupta ilifanya nifutwe kazi | Matukio ya Afrika | DW | 03.10.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Nhlanhla Nene: Mikataba kuhusu Gupta ilifanya nifutwe kazi

Waziri wa fedha wa Afrika Kusini Nhlanhla Nene amesema sababu kuu ya kufutwa kwake kazi ilikuwa kukataa mpango uliopendekezwa wa kujenga viwanda vya nishati ya nyuklia. Mikataba ambayo ingenufaisha familia ya Gupta

Waziri wa fedha wa Afrika Kusini Nhlanhla Nene amesema kuwa alifukuzwa kazi na rais wa zamani Jacob Zuma kwa sababu alikataa kuidhinisha mikataba ambayo ingeinufaisha kifedha familia ya Gupta, ambao ni marafiki wa Zuma wanaotuhumiwa kwa rushwa.

Nene, ambaye alikuwa anatoa ushahidi katika kamati ya uchunguzi ya kimahakama kuhusu ushawishi wa familia hiyo katika masuala ya serikali leo, amesema sababu kuu ya kufutwa kwake kazi ilikuwa kukataa mpango uliopendekezwa wa kujenga viwanda vya nishati ya nyuklia.

Mradi huo ungegharimu hadi dola bilioni 100.

Zuma na familia ya Gupta wanakanusha madai kwamba walikula njama ili kubadilisha matumizi ya fedha za serikali kwa njia zisizofaa.