1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Navalny azikwa mjini Moscow

John Juma
1 Machi 2024

Aliyekuwa kiongozi wa upinzani na aliyefariki dunia akiwa gerezani nchini Urusi, Alexei Navalny, amezikwa mjini Moscow katika maziko yaliyohudhuriwa na maelfu ya wafuasi wake pakiwa na idadi kubwa ya maafisa wa usalama.

https://p.dw.com/p/4d5LA
Urusi, maziko ya Navalny
Waombolezaji kwenye maziko ya Alexei Navalny siku ya Ijumaa (Machi 1, 2024) mjini Moscow.Picha: REUTERS

Maelfu ya waombolezaji walifika katika maziara ya Borisovskoye kumuaga kiongozi huyo aliyekuwa mkosoaji mkubwa wa Rais Vladimir Putin.

Wapendwa wake wamesema alizikwa muda mfupi baada ya ibada ya kanisani iliyofanyika viungani mwa mji wa Moscow.

Soma zaidi: Navalny atarajiwa kuzikwa kusini mwa jiji la Moscow

Navalny, aliyekuwa na umri wa miaka 47,aliaga dunia wiki mbili zilizopita katika gereza alikokuwa amefungwa.

Kulikuwa na idadi kubwa ya polisi wakati wa mazishi hayo yaliyofanyika baada ya mvutano kati ya familia na maafisa kuhusu kukabidhiwa kwa mwili wake.

Mke wake na wanaharakati wenzeke wamemtuhumu Rais Putin kuhusika na kifo chake.