1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

NATO yaitaka China kuchagua, ama magharibi au Urusi

25 Mei 2024

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya kujihami ya NATO Jens Stoltenberg amesema hatua ya China ya kuiunga mkono Urusi ni jambo muhimu mno kwa Moscow katika vita vyake dhidi ya Ukraine.

https://p.dw.com/p/4gHB2
Ukraine | Katibu Mkuu wa Jumuiya ya NATO Jens Stoltenberg
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya kujihami ya NATO Jens StoltenbergPicha: Efrem Lukatsky/AP Photo/picture alliance

Stoltenberg ameliambia gazeti la Ujerumani la Bild kwamba, China haiwezi kusimama pande zote mbili, wakati ikilenga kuimarisha ushirikiano na magharibi, na kwa upande mwingine ikichochea vita barani Ulaya. 

Amesema kuna ongezeko kubwa la mauzo ya vifaa vya mashine na teknolojia nyingine ambazo Moscow inazitumia kutengeneza makombora, vifaru na ndege za kivita ili kuishambulia Ukraine.

Soma pia: Rais Xi wa China akosoa NATO kabla ya ziara yake ya Serbia

Ingawa hakuna rekodi inayoashiria kwamba China inaiuzia Urusi silaha na risasi, lakini mauzo mengine kutoka China kwenda Urusi yameongezeka tangu vita hivyo vilipoanza mnamo Februari mwaka 2022.