1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI:Euro milioni 90 kupambana na Ukimwi,Kifua Kikuu na malaria

14 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CG1W

Mfuko wa Fedha wa Kupambana na Ukimwi,malaria na Kifua kikuu unaidhinisha msaada wa euro milioni 90.7 ili kuimarisha mpango wa kupambana na Ukimwi nchini humo.Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Kenya fedha hizo zitatumika kufadhili mpango huo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.Kiasi cha euro milioni 32.2 kitatolewa katika awamu ya kwanza na kinachosalia kutolewa baada ya miaka miwili ya kwanza.

Mfuko huo ulianzishwa mwaka 2002 na mpaka sasa umepokea jumla ya dola milioni laki tatu na sita kupambana na magonjwa ya Malaria,Kifua Kikuu na Ukimwi.

Wakati huohuo Umoja wa Mataifa unaomba msaada wa euro milioni 12 ili kufadhili mahitaji ya wakimbizi katika kambi za Kakuma na Dadaab zilizoko kaskazini mwa Kenya.Kambi hizo zina jumla ya wakimbizi laki mbili thelathini na moja kutoka mataifa ya Somalia na Sudan.

Watoto katika kambi hizo wako katika hatari ya kuathiriwa na utapia mlo na ukosefu wa damu mwilini.

Kulingana na sheria za Serikali ya Kenya wakimbizi hawaruhusiwi kutafuta kazi nje ya kambi hizo,kulisha mifugo au hata kuhusika na shughuli za kilimo.