MONTEVIDEO : Rais Bush akutana na Rais Vasquez | Habari za Ulimwengu | DW | 10.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MONTEVIDEO : Rais Bush akutana na Rais Vasquez

Rais George W. Bush wa Marekani amekutana na Rais mwenzake wa Uruguay Tebare Vasquez mjini Montevideo kwa mazungumzo yanayotazimiwa kukita kwa kina katika masuala ya biashara wakati maandamano ya umma yakiendelea kuiandama ziara yake ya mataifa matano ya Amerika Kusini.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano wake na rais wa Uruguay rais Bush ametowa wito wa kufikiwa kwa makubaliano ya biashara duniani ambapo amesema biashara huru inaweza kusaidia kupambana na umaskini.

Usalama umeimarishwa kwenye mji mkuu wa Montevideo kufuatia maandamano ya ghasia kabla ya kuanza kwa ziara ya kiongozi huyo wa Marekani.Bush amewasili nchini humo akitokea mjini Sao Paulo nchini Brazil ambapo pia maelfu ya watu waliandama kupinga ziara yake.Mkutano wa Bush na Rais Luiz Lula da Silva wa Brazili umelenga kuendeleza matumizi ya gesi ya methanol kama nishati mbadala na kutafuta njia za kufufuwa mazungumzo yaliokwama ya Shirika la Biashara Duniani WTO.

Wakati huo huo katika ziara inayokwenda sambamba na ya Bush Amerika ya Kusini Rais Hugo Chavez wa Venezuela yuko nchini Argentina ambapo katika maandamano ya umma mjini Buenos Aires amemkejeli Bush kwa kumwita maiti wa kisiasa.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com