1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mlipuko waigeuza Beiru kama uwanja wa vita

Iddi Ssessanga
4 Agosti 2020

Watu wasiopungua 60 wameuawa na karibu 2,750 kujeruhiwa kufuatia mlipuko mkubwa katika bandari ya Beirut. Majengo yameharibiwa na madirisha kuvunjika umbali wa kilomita tano.

https://p.dw.com/p/3gQ8a
Libanon | Gewaltige Explosion in Beirut
Picha: Reuters/I. Abdallah

Mlipuko mkubwa katika bandari iliyopo mji mkuu wa Lebanon Beirut umesababisha vifo vya watu wasiopungua 50 na kujeruhi wengine karibu 2,750 siku ya Jumanne, kulingana na waziri wa afya wa Lebanon.

Haikujulikana mara moja kipi kilisababisha mlipuko huo.

Madirisha yamevunjwa na majengo kuharibiwa katika mlipuko huo ambao kishindo chake kimekwenda umbali wa zaidi ya kilomita tano kutoka eneo la tukio, huku moshi ukitanda mji mzima.

Shirika la Msalaba Mwekundu limesema kulikuwepo na majeruhi wasiopungua 2,200 kutoka na mripuko huo, huku mashuhuda kadhaa wakiripoti kwamba baadhi ya waliojeruhiwa huenda wamefunisha chini ya vifusi.

Gavana wa Beirut aliiamba Televisheni ya ndani: " Sijawahi katika maisha yangu kuona janga lenye ukubwa huu."

Libanon | Gewaltige Explosion in Beirut: Mann wird evakuiert
Majeruhi akiondolewa kwenye eneo la tukio mjini Beirut, Lebanin, Agosti 4, 2020.Picha: Reuters/M. Azakir

'Mpira wa Moto'

"Nyumba yangu imeharibiwa kabisaa," Joachim Paul kutoka wakfu wa Kijerumani wa Heinrich Böll aliiambia DW. "Nilikuwa katika jengo la maduka wakati mlipuko ulipotokea, na nilifikiria kwamba bomu limeripuka ndani ya jengo hilo la maduka."

Paul alisema angekuwa amekaa mezani kwake katika nyumba yake wakati wa mripuko huo angejeruhiwa vibaya.

Soma pia:Mlipuko mkubwa Beirut waua watu 60

Shuhuda moja aliliambia shirika la Habari la Reuters, "Niliona mpira wa moto na moshi ukitanda juu ya anga ya Beirut."

"Watu walikuwa wanapiga mayowe na kukimbia, wakivuja damu. Roshani zimevunjwa kwenye majengo. Vioo vya majengo marefu vimevunjika na kuanguka barabarani."

Watu kadhaa walionekana wakiwa wamelala chini wakiwa majeruhi na hospitali zilitoa wito wa dharura wa kujitolea damu, limeripoti shirika la habari la Associated Press.

Hospitali moja iliripoti zaidi ya wagonjwa 50 waliwasilishwa, na kufikisha ukomo wa uwezo wake.

Libanon | Gewaltige Explosion in Beirut
Watu wakikimbilia maisha yao kufuati mripuko katika eneo la bandari mjini Beirut, Agosti 4, 2020.Picha: Reuters/M. Azakir


'Maghala yalihifadhi vifaa vye uwezekano mkubwa wa kuripuka'

Vituo vya televisheni vya ndani viliripoti kwamba mlipuko huo umetokea kwenye eneo ambako fataki zinauzwa, huku shirika la habari la serikali ya Lebanon NNA likinukuu duru za usalama zikisema maghala hayo huenda yalikuwa yamehifdhi viripuzi.

Mkuu wa usalama Abbas Ibrahim alithibitisha kwamba kulikuwepo na maghala katika eneo hilo yaliohifadhi "vifaa vyenye uwezekano mkubwa wa kulipuka," bila kufafanua juu ya iwapo hili lilimaanisha silaha au fataki. Ibrahim alisema vifaa "vilikamatwa maiaka kadhaa iliyopita."

Soma pia: Waandamanaji warejea mitaani Lebanon kwa kutumia magari

Shirika la Msalaba Mwekundu la Lebanon lilisema "mamia" walijeruhiwa na kutweet kuwa zaidi ya timu 30 zilikuwa zinaitikia tukio hilo.

Waziri Mkuu Hassan Diab alitangaza kwamba siku ya Jumatano itakuwa siku ya kitaifa ya kuomboleza kwa ajili ya wahanga wa mlipuko huo, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya ndani, huku Rais Michel Aoun akiitisha mkutano wa dharura na Baraza la Usalama wa Taifa.

Katika hotuba kupitia televisheni ya taifa, Diab ameapa kwamba wanaohusika na mlipuko huo "watalipa gharama."

Libanon | Gewaltige Explosion in Beirut
Mwanaume akipigwa na butwaa kwenye eneo la mripuko huo.Picha: Getty Images/AFP/A. Amro

Jumuiya ya kimataifa yaitikia

Ikulu ya White House ilitangaza kwamba Marekani ilikuwa inafuatilia mlipuko huo kwa karibu na ilikuwa tayari kutoka "msaada wote unaowezekana." Umoja wa Ulaya, Ufaransa na Iran pia zilitangaza zitaisadia Lebanon katika namna yoyote inayohitajika.

Baada ya mlipuko huo, Israel ilisema haihusiki vyovyote. Waziri wa mambo ya kigeni wa Israel Gabi Ashkenazi aliiambia televisheni ya Israel kwamba anaamini mlipuko huo huenda ulisababishwa na moto, na kuhimiza "tahadhari juu ya uvumi." Israel pia iliongeza sauti yake kwa zile zinatoa msaada wa kiutu.

Hali ya wasiwasi imekuwa kubwa kati ya mataifa hayo jirani, baada ya Israel kusema ilizuwia jaribio la wapiganaji wa Hezbollah kujipenyeza nchini mwake. Hezbollah na Israel wamepigana vita mwaka 2006.

Lebabon pia kwa sasa imo katika mzozo mkubwa wa kiuchumi, ambapo watu wengi wanaandamana katika miezi y akaribuni kupinga hali mbaya ya kifedha.