1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya waanza Brussels

23 Machi 2023

Mkutano wa Kilele wa siku mbili wa viongozi wa Umoja wa Ulaya umeanza leo mjini Brussels ajenda kuu ikiwa ni kuhakikisha uchumi wa eneo hilo unaweza kuwa katika ushindani katika siku zijazo.

https://p.dw.com/p/4P70S
Belgien Brüssel | EU-Gipfel | Rede Wolodymyr Selenskyj im EU-Parlament
Picha: Kenzo Tribouillard/AFP/Getty Images

Kanda hiyo kwa wakati huu inatatizwa mambo mengi ambayo viongozi hao wanapaswa kuyaweka  mezani ikiwemo mfumuko wa bei, nishati ghali, uhaba wa wafanyakazi na mapungufu ya uwekezaji.

Katika mkutano huo kunatarajiwa kuwa na msururu wa rasimu za sheria zenye kufanikisha mabadiliko katika sera ya viwanda, ikiwemo magaeuzi katika soko la nishati ya umeme, msukumo wa kufanikisha upatikanaji zaidi wa malighafi na kuhama kutoka katika kuitegema China kama chanzo cha teknolojia ya nishati safi.