Mkutano kuhusu ukimwi wafunguliwa leo Mexico City | Habari za Ulimwengu | DW | 03.08.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Mkutano kuhusu ukimwi wafunguliwa leo Mexico City

Mexico-City:

Kabla ya kuanza mkutano mkubwa wa kimataifa kuhusu UKIMWI nchini Mexico , maelfu ya wanaharakati wameandamana kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, kulaani ubaguzi dhidi ya wahanga wa ugonjwa huo. Jumla ya washiriki 22.000-wanasayansi, waandaaji sera na watoaji huduma -wanakusanyika kuanzia leo mjini Mexico City kwa mkutano wa siku sita utakaofunguliwa na katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon. Pia rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton anatarajiwa kushiriki. Watu wapatao 33 milioni duniani kote wamekumbwa na ugonjwa huo.

Katika bara la Afrika kusini mwa jangwa la Sahara Ukimwi ni chanzo cha vifo vya mamilioni wenye ukosefu wa dawa na matibabu ya kutosha.

Duniani kote, watu milioni mbili hufariki dunia kila mwaka kwa sababu ya Ukimwi, wakati mambukizo mapya yanafikia karibu watu milioni mbili na nusu. Nchini Marekani maafisa wanasema watu 56.000 wanaambukizwa ukimwi kila mwaka,ikiwa ni asili mia 40 zaidi kuliko makadirio ya hapo awali nchini humo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com