Mkutano kuhusu kuwarejesha makwao wakimbizi wafanyika Goma
27 Julai 2010Matangazo
Mkutano unaolenga kupanga mikakati ya kuwarudisha nyumbani wakimbizi kutoka Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, unafanyika mjini Goma mashariki mwa nchi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mkutano huo umewakusanya pamoja wajumbe kutoka Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia wakimbizi, UNHCR. Mkutano huo unafuatia ule uliofanyika mjini Kigali, Rwanda, mwezi Februari mwaka huu.
Mwandishi wetu aliyeko Goma, John Kanyunyu ametutumia ripoti ifuatayo.
Mwandishi: John Kanyunyu
Mhariri: Josephat Charo