1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Meli ya mafuta ya Iran yakamatwa Gibraltar

5 Julai 2019

Ni tukio linaloweza kuuzidisha mvutano kati ya Iran na nchi za Magharibi ambapo tayari Iran imeshatahadharisha kwamba itazikamata meli za mafuta za Uingereza endapo meli ya Grace 1 haitoachiwa

https://p.dw.com/p/3LclX
Öltanker auf dem Weg nach Syrien in Gibraltar festgesetzt
Picha: Reuters/Stringer

((Wanajeshi wanamaji wa Uingereza jana waliikamata meli kubwa ya mafuta ya Iran katika eneo la Gibraltar ikituhumiwa kusafirisha mafuta nchini Syria na kukiuka vikwazo vilivyowekwa na Umoja wa Ulaya dhidi ya Syria. Wafanyakazi wa meli hiyo wanahojiwa kama mashahidi, katika juhudi za kutafuta malezo juu ya mzigo ulioko kwenye meli hiyo na kituo cha mwisho ulikokusudiwa kupelekwa.

Tukio la kukamatwa meli kubwa kabisa inayosadikiwa ilikuwa inaelekea Syria kupitia Gibraltar ni la jana na leo ripoti zinaeleza mabaharia wote ndani ya meli hiyo wameshikiliwa na wanahojiwa kutowa ufafanuzi na maelezo zaidi kuhusu meli hiyo na safari yenyewe kwa ujumla,kwa mujibu wa msemaji wa upande wa Uingereza. Meli inayoitwa Grace 1 ilikamatwa na wanajeshi wa majini wa Uingereza ikisadikiwa ilikuwa ikijaribu kusafirisha mafuta nchini Syria.

Öltanker Grace 1 vor Gibraltar gestoppt
Picha: picture-alliance/B. Birchall

Msemaji kutoka upande wa Uingereza amesema wafanyakazi  28 waliobakia ndani ya meli hiyo wengi walikuwa ni raia wa India,na baadhi wakiwa wapakistan na Waukraine. Polisi na maafisa wa forodha bado wako ndani ya meli hiyo wakiendesha uchunguzi lakini wanajeshi wa majini wa Uingereza wameondoka.Meli hiyo inatajwa kwamba ilingia kwenye eneo la bahari lililoko chini ya milki ya Uingerea baada ya kusafiri kipindi kirefu katika eneo la Afrika ikitokea upande wa Ghuba.Data za usafiri wa meli hiyo zilizotathminiwa na shirika la habari la Reuters zinaonesha kwamba meli hiyo ilipakia mafuta kwenye pwani ya Iran ingawa nyaraka zinaonesha kwamba mafuta hayo yanatokea nchini Iraq.

Mvutano waanza

Iran leo imeitaka Uingereza kuiachia mara moja meli hiyo ikiituhumu nchi hiyo kufuata maagizo ya Marekani. Kamanda wa ngazi ya juu wa Iran amesema litakuwa jukumu la nchi yake kukama meli za mafuta za  Uingereza ikiwa meli yake haitoachiwa.

Hatua ya kukamatwa meli hiyo huenda ikazidisha malumbano na mvutani kati ya nchi za magharibi na Iran na hasa kwasababu maofisa wa Gibraltar walioikamata meli hiyo walichukua uamuzi huo chini ya mamlaka ya Umoja wa Ulaya iliyoiwekea vikwazo Syria tokea kipindi cha miaka mingi.

Öltanker auf dem Weg nach Syrien in Gibraltar festgesetzt
Picha: Reuters/J. Nazca

Katika taarifa serikali ya Gibraltar imesema ina sababu za msingi za kuamini kwamba meli hiyo imebeba mzigo wa mafuta ghafi ikiyasafirisha katika kiwanda cha kusafisha mafuta cha Banyas nchini Syria. Waziri wa mambo ya nje wa Spain Joseph Borrell akizungumzia suala hili amesema meli hiyo imekamatwa kwa ombi la Marekani.

''bila shaka tilikuwa tunafahamu kuhusu operesheni hii.walinzi walikuwa wakifanya doria kwenye eneo hilo lakini tunachunguza mazingira ya tukio hili lilivyotokea. Hili ni ombi lilotolewa na Marekani kwa Uingereza.tunachunguza kuona jinsi suala hili litakavyoathiri uhuru wetu kwa maana ya kwamba ni tukio lililofanyika katika eneo letu la bahari,ambalo tunafahamu liko chini ya himaya ya Uhispania''

Meli hiyo imekamatwa kilomita nne kutoka kusini mwa Gibraltar eneo ambalo linaangaliwa kama liko chini ya Uingereza ingawa uhispania ambayo inadai hilo ni eneo lake,inasema walioikamata meli hiyo ni Wahispania.

Mwandishi: Saumu Mwasimba

Mhariria: Josephat Charo

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW