1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Africa Cup Fußball | Südafrika vs. Nigeria
Picha: Getty Images/AFP/P. Magakoe

Mauritania yafuzu kucheza fainali za AFCON

Sekione Kitojo
19 Novemba 2018

Mauritania  yafuzu kwa mara  ya kwanza  kucheza  AFCON , Taifa  Stars  Tanzania  kuteleza  si  kuanguka, bado  nafasi  ipo  ya kucheza  fainali  hizo nchini Cameroon.

https://p.dw.com/p/38Xff

Barani  Afrika  mauritania  imefuzu  kucheza  katika  fainali  za kombe  la  mataifa  ya  Afrika  jana  Jumapili  wakati  walipoishinda Botswana  na  kunyakua  nafasi  katika  fainali  za  mwakani  za kombe  la  mataifa  ya  Afrika nchini  Cameroon.

Mauritania  ni  moja kati  ya  nchi  13 ambazo  zimekwisha  fuzu  katika  kinyang'anyiro hicho  kitakachozikutaninisha  timu  24. Timu  nane  kati  ya  hizo zimefuzu  mwishoni  mwa  juma  hili, zikiongozwa  na  mabingwa  wa zamani  Nigeria, Ivory Coast, Morocco  na  Algeria.

Fußball Afrika Cup 2015 Bertrand Traoré
Picha: Getty Images/AFP/K. Desouki

Ivory Coast , mabingwa   wa  Afrika mwaka 2015, walihakikisha nafasi  yao ya kufuzu  walipotoka  sare  ya  bao 1-1  na  Guinea  jana na  matokeo hayo  yakawapa nafasi  wote  ya  kufuzu.  Morocco  ilijihakikishia nafasi  ya  kufuzu baada  ya  Malawi  kwa  mshangao  kupoteza mchezo  wake  dhidi  ya  Comoro  kwa  mabao 2-1.

Libya ina  nafasi  ya  kufuzu na  inakabiliana  na  Afrika  kusini mwezi Machi na  kujiunga  na  Nigeria  katika  kundi  lao kucheza  katika fainali. hata  hivyo  Libya inahitaji  kushinda  wakati Afrika  kusini inahitaji  sare. 

Gabon  - Ägypten gegen Marokko beim Africa Cup of Nations
Picha: picture-alliance/AA/F. Kotb

Burundi  inahitaji  pia  sare  nyumbani  dhidi  ya Gabon , wakati  Lesotho  pia  nayo  inaweza  kufuzu  iwapo itaishinda  Cape Verde na  Tanzania  kushindwa  na  Uganda , baada ya  jana  Tanzania  kuangukia  pua  kwa  kufungwa  bao 1-0 dhidi  ya Lesotho.

 

Mwandishi: Sekione  Kitojo / dpae / ape / afpe / rtre

Mhariri:  Yusuf , Saumu