Mataifa matano kutuma askari kikosi cha kimataifa Haiti
1 Machi 2024Kikosi hicho kimeundwa ili kuwasaidia polisi wa taifa hilo la Karibiani kupambana na makundi ya magenge ya uhalifu.
Mataifa hayo ni Benin, Chad, Bahamas, Bangladesh na Barbados.
Haiti: Haiti kufanya uchaguzi Agosti 2025
Mnamo mwezi Oktoba, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliidhinisha kutumwa kwa kikosi maalum nchini Haiti chini ya uongozi wa Kenya, katika juhudi za kulisaidia jeshi la polisi katika taifa hilo masikini la Karibiani ambalo limegubikwa na machafuko.
Lakini hadi sasa kikosi hicho bado hakijawasili, baada ya mahakama moja nchini Kenya kuzuia kutumwa kwa maafisa wa polisi 1,000 wa Kenya.
Waziri Mkuu wa Haiti, Ariel Henry, aliwasili nchini Kenya siku ya Alhamis (Februari 29) kufuatilia suala hilo na mwenyeji wake, Rais William Ruto.