MARIETTA : Misa kwa Mkenya na mabinti zake waliouwawa | Habari za Ulimwengu | DW | 06.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MARIETTA : Misa kwa Mkenya na mabinti zake waliouwawa

Mamia ya watu wamehudhuria misa ya kumbukumbu kwa ajili ya mhamiaji wa kike wa Kenya ambaye amekutikana ameuwawa na mabinti zake wawili nyumbani kwao katika jimbo la Georgia nchini Marekani.

Jamii ya Wakenya katika eneo hilo walikusanyika hapo jana kumkumbuka Gakuny Kuria mwenye umri wa miaka 46 na wanawe Isabela mwenye umri wa miaka 19 na Annabelle mwenye umri wa miaka 16.Watu hao watatu walikutikana wakiwa wamekufa Jumaatano iliopita wakiwa nyumbani kwao.Mtoto wa kiume wa mwanamke huyo Peter Jeremy Kuria mwenye umri wa miaka 7 na binamu yake Peter Thiande mwenye umri wa miaka 8 wamekutikana wakiwa hawana fahamu na wamelazwa hospitali.

Familia na marafiki pia wamechangisha michango kugharamia gharama za kupeleka maiti nyumbani kwa mazishi.

Hakuna mtu aliekamatwa kutokana na mauaji hayo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com