Marekani yawawekea vikwazo jamaa wa Maduro huku hofu ikizidi
12 Desemba 2025
Matangazo
Taarifa ya Waziri wa Fedha wa Marekani Scott Bessent imesema waliowekewa vikwazo ni wapwa watatu wa mke wa Maduro, Cilia Flores, akidai kuwa wawili kati yao ni "walanguzi wa dawa za kulevya wanaofanya shughuli zao ndani ya Venezuela."
Taarifa hiyo imeongeza kuwa Maduro na aliowataja kuwa "washirika wake wa uhalifu" wameingiza dawa nyingi za kulevya Marekani ambazo ni sumu kwa raia.
Washington imechukua hatua hiyo, huku Ikulu ya White House ikisema itaifikisha Marekani meli ya mafuta iliyokamatwa na vikosi vyake hivi karibuni nje kidogo ya pwani ya Venezuela.
Hayo yanajiri wakati kukiwa na hofu ya mzozo unaoendelea kufukuta kati ya nchi hizo mbili.