1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Mapigano makali yaitikisa Gaza ikiwemo mji wa Rafah

Saleh Mwanamilongo
13 Mei 2024

Jeshi la Israel limepambana leo Jumatatu na wanagambo wa Hamas huko Gaza, ikiwa ni pamoja na kusini mwa mji wa Rafah.

https://p.dw.com/p/4fo3X
Mapigano Ukanda wa Gaza.
Mapigano Ukanda wa Gaza.Picha: AFP

Makabiliano hayo yameshuhudiwa, licha ya onyo la Marekani kwa Israel dhidi ya kufanyauvamizi kamili kwenye mji huo wa Rafah, uliofurika watu.

Kwa mujibu wa waandishi habari na mashuhuda, mapigano pia yalizuka katika maeneo ya kaskazini na kati ya Ukanda wa Gaza. Huku Israeli ikijiandaa kuadhimisha siku ya Uhuru wake hapo kesho.

Hii leo, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amehutubia hafla ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa na kusema kwamba vita vya uhuru wa Israel bado havijaisha na vinaendelea hata leo. Netanyahu amesema Israel imedhamiria kushinda vita hivyo.

Kuliripotiwa mashambulizi ya helikopta na mizinga mikubwa mashariki mwa mji Rafah, pamoja na mapigano katika kambi ya wakimbizi ya Jabalia kaskazini mwa ukanda Gaza na kitongoji cha Zeitun cha mji mkuu wa Gaza City.