Ni ugonjwa wa kudumu, unaohusishwa kwa kiwango kikubwa na umasikini, tabia yake kuu ni kushambulia mifumo ya mawasiliano kati ya ubongo na mwili, lakini ugonjwa huu huchukua muda mrefu hadi kujitokeza katika mwili wa mgonjwa.
Lakini ni ugonjwa ambao ukichelewa matibabu utakuacha na ulemavu wa kudumu. Wengi huchelewa kwani wanaamini ukoma unatokana na kulogwa. Kumbe ni ugonjwa wa maambukizi.