Maoni ya Wahariri juu ya Mashariki ya Kati na ziara ya Obama | Magazetini | DW | 20.11.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Maoni ya Wahariri juu ya Mashariki ya Kati na ziara ya Obama

Pamoja na masuala mengine waharriri wa magazeti wanatoa maoni juu ya ziara ya Rais Obama nchini Myanmar, mgogoro wa Mashariki ya Kati na juu ya mkutano wa Mawaziri wa fedha wa Umoja wa Ulaya.

Wanajeshi wa Israel wakiwatayari kuingia Gaza?

Gaza Israel Luftangriff Panzer

Juu ya mgogoro wa Mashariki ya Kati gazeti la "Neue Osnabrücker linaitahadharisha Israel kwamba hali imebadilika katika Mashariki ya Kati baada ya mapinduzi katika nchi za kiarabu.Kwa mfano viongozi wa Misri wanaonyesha msimamo wa uhakika.Hali hiyo inaweza kuwa hatari kwa Israel. Ndiyo sababu nchi za magharibi zinatumia uwezo wote ili kuleta suluhisho kwa njia ya mazungumzo.

Gazeti la "Badische" pia limeandika juu ya vita vya Gaza.Mhariri wa gazeti hilo anasema, watu Milioni tatu wanaishi na hofu wakati wote nchini Israel. Lakini nje ya nchi hiyo hakuna anaeyatambua hayo. Ni kinyume chake, kwamba jumuiya ya kimataifa inahamaki kwa kiwango kikubwa ikiwa Israel inachukua hatua ili kujihami na ikiwa inalipiza kisasi.Ni wazi kwamba kutokana na nguvu kubwa za kijeshi dhidi ya Wapalestina, Israel haraka sana inajiweka katika kizimba cha mkosaji. Mhariri wa gazeti la "Badische" anasema ni jambo la kusikitisha katika mgogoro wa Mashariki ya Kati, usiokuwa na mwisho, kwamba ,mtanziko unaoikabili Israel hautambuliwi vizuri.

Gazeti la "Der Neue Tag" linauzingatia uhusiano baina ya Marekani na Myanmar katika muktadha wa ziara ya Rais Obama. Mhariri wa gazeti hilo anaeleza:

Ili kujinasua na kuondokana na kabali ya China,Mynmar inahitaji rafiki mwenye nguvu ili kuukabili uzito wa China. Rafiki huyo bila shaka atatoka magharibi, na hasa ni Marekani.
Mawaziri wa fedha wa nchi za Umoja wa Ulaya wanakutana leo kuamua juu ya msaada mwingine kwa Ugiriki. Lakini mhariri wa gazeti la "Der Tagesspiegel" anatahadharisha:

Anaetaka hatua kali zuchukuliwe,kwa mfano, kuiachie Ugiriki ianguke, anapaswa kuukumbuka mgogoro uliosababishwa na benki ya Lehman Brothers nchini Marekani. Utawala wa Marekani ulifikiri ungeliweza kuichukua benki hiyo. Lakini ilisambarika

na kusababisha mgogoro mkubwa wa kiuchumi duniani kote.
Mhariri wa "Der Tagesspiegel" anasema anatumai kwamba mawaziri wa fedha wa nchi za Umoja wa Ulaya hawatafanya kosa la kupitisha maamuzi ya patapotea!

Na tunakamilisha kwa maoni ya gazeti la "Münchner Merkur" juu ya mwito uliotolewa kwa watu wa Ulaya ,kuwashauri watumie busara katika kuukabili mgogoro wa madeni.

Mhariri wa gazeti hilo anafafanua

Mgororo wa madeni unazitia hafo jamii zote,maalfu ya watu wametumbikia katika umasikini,na hali ya kutamauka inasababisha tuhuma zisokuwa na msingi.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel anasingiziwa kuwa ni chanzo cha matatizo ya watu nchini Ugiriki,Ureno na hata Italia.Ni kutokana hali hiyo kwamba Rais Joachim Gauck wa Ujerumani na Napolitano wa Italia wanawataka wanasiasa waepuke kukaanga mbuyu!

Mwandishi:Mtullya abdu.Duetsche Zeitungen/

Mhariri:Abdul-Rahman