1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni: Olaf Scholz alishindwa kumnyamazisha Mahmoud Abbas

18 Agosti 2022

Kufafanisha mauaji ya wayahudi na matukio mengine ni jambo linalopaswa kukanushwa haraka sana nchini Ujerumani. Kuchelewa kwa kansela Olaf Scholz kujibu haraka kunaonesha mambo hayaendi sawa, anaandika Judith Hofmann.

https://p.dw.com/p/4FkVP
Berlin | Pressekonferenz: Olaf Scholz und Mahmoud Abbas
Picha: Wolfgang Kumm/dpa/picture alliance

Tunachoweza kusema juu ya kunyamaza kimya kwa kansela wa Ujerumani juu ya kufananishwa kwa mauaji dhidi ya Wayahudi-Holocaust ni kwamba alikuwa hana la kufanya. Kansela Scholz alitoa macho na kuzatama mbele tu akiwa amekasirika. Hata hivyo hakutoa kauli ya kupinga baada ya rais wa mamlaka ya ndani ya Palestina Mahmood Abbas alipotoa kauli ya uchokozi pale aliposema kwamba tangu mwaka 1947 Israel imefanya mauaji ya kimbari mara 50 kwenye miji 50 ya wapalestina. Alisema Israel imetenda mauaji ya mfano wa Holocaust mara 50. Baada ya hapo msemaji wa kansela aliufunga mkutano na waandishi habari.

Jambo moja linapaswa kuwa wazi kabisa, Kansela yeyote wa Ujerumani hapaswi kumwachia mgeni yeyote kukanusha kufanyika kwa maangamizi ya wayahudi, kujaribu kulinganisha au kwa namna nyingine yoyote kujaribu kupaka matope kumbumbuku juu ya uhalifu mkubwa uliowahi kufanyika katika historia, hususan akifanya hivyo kwenye ardhi ya Ujerumani.

Soma pia: Scholz akosolewa kwa jinsi alivyojibu kauli ya Abbas kuhusu Holocaust

Maangamizi ya wayahudi - pengine inabidi kulikumbushia hili lisikike tena nchini Ujerumani - yalipangwa mjini Berlin.Chama cha mafashisti cha National Socialist Germany ndicho kilichohusika na kuuliwa kwa Wayahudi milioni sita. Kwa hivyo mpaka leo, ni wajibu wa serikali zote za Ujerumani kuendeleza kumbukumbu juu ya wahanga hao.

Ni kwa kiasi gani bado wajerumani wanakumbuka?

Inavyoonekana utamaduni huo wa kumbukumbu unakwenda mrama. Hakuna njia nyingine ya kueleza kwa nini Scholz alinyamaza kimya wakati neno ubaguzi wa rangi (Apartheid) lilipotumika. Neno hilo ni la utata mkubwa ambalo serikali ya Israel inalilaani kuwa ni chuki dhidi ya Wayahudi - mara ya hivi karibuni ikiwa ni baada ya shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International kulitumia katika ripoti yake.

Kommentarbild Autorenbild Sarah Judith Hofmann
Mwandishi wa DW, Sarah Judith Hofmann.Picha: DW

Ni neno la utata miongoni mwa wasomi wa Marekani, Israel na Ujerumani. Hata hivyo ni muhimu kwamba kansela  wa Ujerumani amesisitiza kuwa ni muhimu kwamba serikali ya Ujerumani hailitumii neno hilo apartheid yaani ubaguzi. Inavyoelekea Kansela Scholz alikuwa ametayarishwa vizuri kuhusiana na hili.

Soma pia: Kiongozi wa Palestina Abbas akutana na waziri Gantz wa Israel

Lakini inakuaje kwamba hakuweza kumtarajia Mahmoud Abbas kufananisha hali na mauaji ya wayahudi? Na kwa kweli hii si mara ya kwanza kwa Mahmoud Abbas kutumia kauli zisizokubalika ili kutafuta kuungwa mkono.

Na hii inadhihirisha hali ya sintofahamu.

Si lazima kwa serikali ya Ujerumani kuainisha istilahi zinazojadiliwa katika muktadha wa mgogoro wa mashariki ya kati. Istilahi za utata zinazotumiwa siyo tu na Mahmoud Abbas, bali pia na Wapalestina wengine na mashirika maarufu ya kutetea haki za Binadamu. Hata hivyo mpaka utakuwa umevukwa itakapohusu kuwakumbuka Wayahudi milioni  sita walioangamizwa. Hapa, Ujerumani inao wajibu na haipaswi kunyamaza kimya.

Ukweli ni kwamba kansela Olaf Scholz hakumjibu haraka Mahmoud Abbas ili kupinga alichosema, amesababisha madhara makubwa kwa Ujerumani siyo tu miongoni mwa Waisraeli. Hilo halipaswi kusamehewa.

Baada ya mkutano na waandishi wa habari, kansela Scholz aliandika kwenye mtandao wa Twitter. Alisema kuwa amekasirishwa na  kauli mbaya alizotoa rais wa Palestina Mahmoud Abbas. Bwana Scholz amesema kwa wajerumani, kulinganisha mauaji ya wayahudi na hali zingine ni jambo lisilokubalika.

Soma pia: Kiongozi wa Palestina aondoa makubaliano yake na Israel na Marekani

Scholz amelaani kila kitendo cha kujaribu kukanusha maangamizi ya Wayahudi. Hata hivyo Kansela Scholz alichelewa kutoa kauli hiyo. Kashfa ilishafika Israel ambako kwa sasa tayari pana hali ya mvutano katika Mashariki ya Kati. Waziri mkuu wa Israel Yair Lapid ambaye mwenyewe ni mtoto wa mhanga wa Holocoust, amesema historia haitamsamehe Abbas.

Mahmoud Abbas si mwakilishi wa Wapalestina wote.

Hapana haja ya kuendelea kuyazungumzia maneno aliyosema Mahmoud Abbas. Ni ya fedheha na aibu. La kutilia maanani zaidi ni kwamba maneno hayo yanawaathiri Wapalestina wanaostahili kupiga kura kwa mara nyingine. Miaka 16 imeshapita tangu Wapalestina wapige kura kwa mara ya mwisho. Wapalestina wanastahili kumchagua mtu atakayewawakilisha duniani.

Baada ya mkutano na wandishi habari Abbas angeliweza kuhakikisha kwamba mazungumzo yanatuama juu ya shambulio la ndege lililofanywa na jeshi la anga la Israel. Watoto watano waliuliwa kwenye Ukanda wa Gaza. Na siyo kama ilivyodaiwa na Israel hapo awali kwamba kombora la wapiganaji wa kipalestina lilikwenda mrama! Badala yake Abbas anazipaka matope kumbukumbu za wahanga wa Holocaust, na pia anahujumu hadhi ya wapalestina wote ambao hawako tayari kuilinganisha na hali zingine yaani Wapalestina wanaotaka kuishi kwa amani na Waisraeli.