Kiongozi wa Palestina aondoa makubaliano yake na Israel na Marekani | Matukio ya Kisiasa | DW | 20.05.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Kiongozi wa Palestina aondoa makubaliano

Kiongozi wa Palestina aondoa makubaliano yake na Israel na Marekani

Kiongozi wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas amesema Palestina haitazingatia tena makubaliano yoyote yaliotiwa saini na Israeli na Marekani kufuatia ahadi ya Israel ya kunyakua eneo Ukingo wa Magharibi.

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas amesema kuwa vugu vugu la ukombozi la Palestina na serikali ya Palestina, hazizingatii tena makubaliano yote yaliotiwa saini na maelewano na serikali ya Israel na Marekani ikiwa ni pamoja na makubaliano ya kiuslama.

Haikubainika mara moja jinsi tangazo hilo lililotolewa jana jioni wakati wa mkutano wa uongozi wa Palestina litakavyotekelezwa. Makubaliano ya Oslo na mengine katika miaka ya tisini yalibuni mamlaka ya Palestina na kusimamia uhusiano wake wa kisiasi, kiuchumi na kuisalama na Israel.

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas ailaumu Marekani

Isarel Vogel auf Stacheldraht

Eneo la Gaza lililowekwa uzio wa waya

Kiongozi huyo amenukuliwa akisema "Nailaumu Marekani kwa ukandamizaji wa wapalestina na tunaichukulia kuwa mshirika mkubwa na wa kimsingi wa serikali iliyo mamlakani ya Israeli katika maamuzi na vitendo vyote vibaya dhidi ya haki za raia wetu." Pia ametangaza kuwa Palestina itaimarisha kampeini yake ya kujiunga na mashirika mengine ya kimataifa kama taifa mwanachama katika kuikaidi Marekani.

Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu aliapa kunyakuwa bonde la Jordan na makazi ya wayahudi katika ukingo wa Magharibi kuambatana na mpango wa rais Donald Trump wa Mashariki ya Kati ambao unainufaisha zaidi Israel na kupingwa wa Wapalestina.

Netanyahu aliunda serikali mpya ya Israel mwezi huu pamoja na mpinzani wake wa zamani Benny Gantz kufuatia chaguzi tatu na mkwamo wa Zaidi ya mwaka mmoja. Makubaliano ya pamoja yanamruhusu Netanyahu kuwasilisha pendekezo la unyakuzi huo kwa serikali mapema hata kuanzia Julai mosi.

Bado haijabainika wazi iwapo Abbas ambaye alitoa vitisho kama hivyo katika siku za nyuma atatimiza kitisho cha tangazo lake la hivi karibuni. Ushirikiano wa kiuslama unamnufaisha Abbas pamoja na Israeli kwa kuwa unalenga Zaidi kundi lenye itikadi kali la Hamas ambalo ni mpinzani wake mkuu.