1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni: Messi ndie bora zaidi kombe la Dunia 2022

Lilian Mtono
19 Desemba 2022

Nyota wa Argentina anastahili kutajwa kama mchezaji bora kabisa wa kiume wa soka, na sio tu kutokana na makombe aliyoyapata, bali pia ni kwa namna anavyolisakata kabumbu.

https://p.dw.com/p/4L9iW
FIFA Fußball WM 2022 in Katar | Finale Argentinien - Frankreich
Picha: Manu Fernandez/AP Photo/picture alliance

Hatimaye ametimiza ndoto yake! Heshima na ndoto kubwa na ya mwisho kwa Lionel Messi imetimia baada ya timu yake ya taifa ya Argentina kubeba Kombe la Dunia. Ni kipi kingine anachokihitaji??

 Hakika sasa anaweza bila ya mashaka yoyote kutambuliwa kama mchezaji bora kabisa wa soka wa muda wote.

Ndio. Anastahili, ingawa Pele, mchezaji nguli wa zamani wa Brazil aliyeshinda kombe la Dunia mara tatu bado anasalia kuwa bora zaidi kwa kuwa hakuna aliyeivunja rekodi yake.

 Lakini hata hivyo soka lilikuwa la tofauti katika kipindi hicho cha mwaka 1958, 1962 na 1970. Messi kwa upande wake amecheza katika kipindi cha ushindani mkali, wenye mechi nyingi, ngumu na zenye shinikizo kubwa.

Soma zaidi:Argentina yanyakua ubingwa

Ameng'ara katika kipindi chote akiwa uwanjani, ameiwezesha Barcelona kushiriki mara nne michuano ya Klabu bingwa Ulaya ama Champions na ubingwa wa ligi ya Uhispania mara 10.

 Ameiongoza pia Argentina kwenye michuano ya Copa America mwaka jana. Messi aidha ana rekodi ya kushinda mara saba tuzo ya mwanasoka bora ulimwenguni ya Ballon d'Or.

Messi pia amethibitisha kuwa na uwezo wa kucheza bila ya matatizo yoyote akiwa na klabu tofauti na Barcelona aliyodumu nayo kwa muda mrefu, na hasa baada ya kuisaidia klabu yake ya sasa ya Paris Saint-Germain kuchukua ubingwa wa ligi ya Ufaransa msimu uliopita.

Maajabu yaliyoko kwenye miguu yake.

Lakini sio tu makombe aliyoshinda Messi, bali hata uchezaji aliouonyesha kwenye michuano hii ya Kombe la Dunia, unamaliza moja kwa moja ubishi kwamba yeye ndio bora zaidi kwa sasa.

Fußball WM 2022 | Argentinien - Frankreich | Lionel Messi
Mcheziji wa timu ya Argentina Lionel MessiPicha: Tom Weller/picture alliance/dpa

Mamilioni ya watoto kote ulimwenguni wanasemawanavutiwa na soka kwa sababu ya Messi, Kijana mdogomdogo wa umbo, mwenye aibu na maajabu kwenye miguu yake.

Hakufanikiwa kuondoka na kiatu cha dhahabu kwenye michuano hii akizidiwa na Kylian Mbappe wa Ufaransa aliyefunga mabao matatu na kuwaingiza miamba hao katika mikwaju ya penati kwenye mechi ya fainali.

Soma zaidi:Ufaransa yatinga fainali baada ya kuibwaga Moroko 2-0

Ingawa hii haimsumbui sana Messi kwa sababu tayari ameshinda tuzo kadhaa kama mchezaji binafsi kwenye michuano mbalimbali.

Pamoja na haya yote, kile chenye uzito zaidi hapa na hasa baada ya machungu ya kuondolewa na Ujerumani katika muda wa ziada mwaka 2014 ni kwamba kwa sasa Messi ni bingwa wa dunia, hata baada ya kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Saudi Arabia katika mechi yao ya ufunguzi.

Mnyenyekevu na mwenye furaha wakati wote.

Hapo nyuma, ilisemekana kwamba marehemu Diego Maradona aliyeichezea Argentina ndio alikuwa bora zaidi kiuchezaji, lakini zuio kutokana na matumizi ya dawa za kulevya, balo la "Mkono wa Mungu" na madai ya kujihusisha na magenge ya uhalifu yaliyoko Italia vyote vinamaanisha kwamba Maradona hastahili sifa hii ya kuwa bora zaidi.

Fußball WM Katar Finale | Argentinien v Frankreich
Lionel Mwssi akishangilia goli la timu yake wakati wa mchezo wa kombe la dunia QatarPicha: Petr David Josek/AP/picture alliance

Licha ya ukweli kwamba Argentina isingeweza kuchukua ubingwa wa Kombe la Dunia mwaka 1986bila bao hilo la Mkono wa Mungu.

Na wakati iliipasa Amerika ya Kusini kusubiri kwa miaka 20, wakati Ulaya ikitawala, sasa Messi ameivunja laana hiyo na kuizuia Ufaransa kulitetea kombe hilo.

Soma zaidi:Morocco "ina njaa ya ushindi zaidi" asema kocha Regragui

Kuna wale ambao bado wanadhani Christiano Ronaldo ndio bora zaidi. Lakini medali ya kombe la dunia zinakosekana kwenye orodha ya mafanikio yake.

Tusisahau pia kulinganisha namna Messi alivyoondoka Barcelona kwa machozi, simanzi na unyenyekevu mkubwa, tofauti na Ronaldo aliyeondoka Manchester United, Real Madrid na Juventus kwa kiburi, majivuni na aliyejawa na ubinafsi.

Ni washindi waKombe la Dunia. Na mechi ya mwisho ya michuano hiyo imemuweka Messi kwenye kiwango cha juu kabisa cha soka.