1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAfrika Kusini

Mamlaka za Johannesburg kulaumiwa kufuatia moto uliowaua 76

6 Mei 2024

Ripoti ya uchunguzi wa ajali ya moto wa mwaka jana katika jengo moja na kuwaua watu 76 nchini Afrika Kusini, umesema mamlaka za mji zinapaswa kuwajibishwa kwa sababu zilifahamu masuala ya usalama hapo kabla.

https://p.dw.com/p/4fYSn
Afrika Kusini | Jengo lililoteketea moto mnamo Agosti 31, 2023
Ripoti ya uchunguzi imebaini kwamba mamlaka zilifahamu hali ya usalama wa jengo hilo kabla ya mkasa wa moto kutokea. Picha: Michele Spatari/AFP/Getty Images

Ajali hiyo ya moto iliyotokea usiku katika jengo la ghorofa tano huko mjini Johannesburg Agosti 31, ilikuwa ni mojawapo ya janga baya zaidi nchini Afrika Kusini.

Watoto wasiopungua 12 walikuwa miongoni mwa watu waliokufa na zaidi ya 76 walijeruhiwa huku baadhi wakilazimika kuruka kupitia madirishani ili kujiepusha na kiama cha moto.

Wengine walielezea kwamba waliwatupa watoto kupitia madirishani kwa matumaini kwamba wangeweza kudakwa na watu walio chini.

Watu wengi waliokufa walichomeka vibaya kiasi cha kushindwa kutambulika baada ya kukwama katika jengo hilo lenye msongamano.

Mamlaka zilitumia vipimo vya vinasaba ili kuitambua miili.