Mamlaka za DRC zatangaza visa 900 vinavyohusiana na Ebola
25 Mei 2026
Matangazo
Taarifa ya Wizara ya Mawasiliano iliyochapishwa kwenye mtandao wa X jana Jumapili imesema kulikuwa na visa 904 na vifo 119 vinavyohisiwa vimetokana na maambukizi yaEbola
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya ulimwenguni, WHO Tedros Adhanom Gebreyesus amethibitisha takwimu hizo na kuongeza kuwa juhudi za ufuatiliaji zinazidi kuimarishwa.
Mamlaka za Kongo hapo kabla zilitangaza zaidi ya visa 700 vya Ebola na zaidi ya vifo 170 vilivyoripotiwa zaidi kwenye jimbo la Ituri ambako ndio kitovu cha mlipuko huo.