1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mamilioni ya watu wakabiliwa na ukosefu wa chakula Chad

Sylvia Mwehozi
11 Aprili 2024

Asasi moja ya Ufaransa inayopambana kutokomeza njaa ya ACF, imeonya jana kuwa takribani watu milioni 3.4 wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu nchini Chad.

https://p.dw.com/p/4edpe
Wakimbizi wa Sudan
Wakimbizi wa Sudan walioko ChadPicha: David Allignon/MAXPPP/dpa/picture alliance

Asasi moja ya Ufaransa inayopambana kutokomeza njaa ya ACF, imeonya jana kuwa takribani watu milioni 3.4 wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu nchini Chad, kufuatia wimbi kubwa la wakimbiziwanaowasili kutokea Sudan wanakokimbia vita.

Taarifa ya asasi hiyo imeeleza kwamba majimbo ya mashariki mwa Chad ni miongoni mwa maeneo yaliyo hatarini zaidi nchini humo na upatikanaji duni wa huduma za msingi na kuwasili kwa wakimbizi kumezidisha hali kuwa mbaya.

Mnamo mwezi Machi, Umoja wa Mataifa ulionya kuwa msaada wa chakula kwa maelfu ya watu wanaokimbia mapigano Sudan, utakosekana kufikia Aprili ikiwa hakuna ufadhili wa kimataifa.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula WFP, limetoa wito wa kukusanywa kwa Dola milioni 242 ili kuepuka janga la kibinadamu na kuendelea kuwahudumia wakimbizi wa Sudan wapatao milioni 1.2.