1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Malkia wa Kilimanjaro mabingwa CECAFA

30 Julai 2018

Timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania Bara Kilimanjaro Queens, imetetea ubingwa wake katika michuano ya CECAFA Women challenge.

https://p.dw.com/p/32KgO

Somalia Frauenfußball
Picha: Getty Images/AFP/M. Abdiwahab

Imetwaa ubingwa baada ya kuwabwaga Ethiopia magoli 4-1 katika uwanja wa Nyamirambo mjini Kigali. Mashindano haya ya wiki mbili yamefikia ukingoni mwishoni mwa juma.

Katika tennis John Isner ndiye bingwa wa mashindano ya Atlanta Open kwa mara ya tano. Isner aliebuka mshindi baada ya kumlaza Ryan Harrison kwa seti tatu za 5-7 6-3 6-4 kwenye fainali iliyochezwa Jumapili.

Isner sasa amekuwa mchezaji wa tano kutoka Marekani kushinda taji moja angalau mara tano baada ya Jimmy Connors, John McEnroe, Pete Sampras na Andre Agassi. Hili ni taji la 14 katika taaluma ya tennis ya Isner ambaye mwezi uliopita alibanduliwa kwenye mashindano ya Wimbledon huko Uingereza kwenye mechi ya nusu ya fainali.

Mwandishi: Jacob Safari

Mhariri: Yusuf Saumu