1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Majeshi ya Israel yamesogea ndani zaidi kaskazini mwa Gaza

30 Oktoba 2023

Vikosi vya Israel vimeendeleza mashambulizi yake kaskazini mwa Gaza na eneo la kati la ukanda huo.

https://p.dw.com/p/4YBsq
Hatua hii ya Israel ya kuendeleza uvamizi wake inayaweka majeshi hayo pande zote mbili za mji wa Gaza.
Hatua hii ya Israel ya kuendeleza uvamizi wake inayaweka majeshi hayo pande zote mbili za mji wa Gaza.Picha: ISRAELI DEFENCE FORCES/via REUTERS

Hayo yanajiri wakati ambapo Umoja wa Mataifa na wahudumu wa afya wameonya kuwa makombora ya angani yanaanguka karibu na hospitali ambapo maelfu ya Wapalestina wakiwemo wengine waliojeruhiwa wamejificha.

Hatua hii ya Israel ya kuendeleza uvamizi wake inayaweka majeshi hayo pande zote mbili za mji wa Gaza, katika kile kilichoitwa na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kama "hatua ya pili" ya vita vilivyoanzishwa na Hamas mnamo Oktoba 7.

Mamia kwa maelfu ya Wapalestina bado wako kaskazini mwa Gaza na hawatoweza kuyakimbia mashambulizi endapo barabara ya kaskazini kuelekea kusini itafungwa.

Jeshi la Israel linasema limewauwa wanamgambo wa Hamas katika operesheni yake hiyo ya kaskazini, baada ya kushambulia majengo na mahandaki.