1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUganda

Mahakama Uganda yapigilia msumari sheria inayopinga LGBTQ

3 Aprili 2024

Mahakama ya katiba nchini Uganda imetupilia mbali shauri lililowasilishwa kupinga sheria dhidi ya mapenzi kati ya watu wa jinsia moja. Kulingana na mahakama, sheria hiyo inalinda utamaduni na hadhi ya watu wa Uganda.

https://p.dw.com/p/4eNTw
Uganda  LGBTQ
Mwanaume wa Uganda akiwa ameshikilia bango la kuunga mkono mapenzi ya jinsia mojaPicha: ASSOCIATED PRESS/picture alliance

Maamuzi ya mahakama ya katiba yenye kurasa 200 yamesomwa kwa muhtasari, naibu jaji mkuu Richard Buteera  akinukuu dondoo mbalimbali zilizowapelekea kufikia maamuzi hayo.

Kulingana na hoja ziliwawasilishwa katika shauri, walalamishi walitaja sababu kadhaa za kupinga sheria hiyo wakitaka itupiliwe mbali.Museveni asaini sheria ya mapenzi ya jinsia moja

Mojawapo ya hoja ni kwamba bunge halikufuata utaratibu stahiki katika kujadili na kupitisha muswaada ulioishia katika rais Museveni kusaini sheria hiyo.

Uganda | Maandamano ya kupinga LGBTQ
Waandamanaji wakiwa wameshikilia mabango ya kuunga mkono hatua ya Rais Yoweri Museveni kutia saini mswada wa kupinga ushoga kuwa sheria mjini Kampala.Picha: Ronald Kabuubi/dpa/picture alliance

Soma: Mahakama ya Uganda yaanza kusikiliza pingamizi kuhusu sheria kali dhidi ya ushoga

Aidha umma haukuhusishwa kutoa maoni yao ila sheria hiyo ilipitishwa baada ya kujadiliwa kwa siku sita tu badala ya 45. Lakini kwa msingi wa hoja ya kulinda utamaduni na hadhi ya Uganda na Afrika jaji Richard Buteera ametamka hivi, "tunakataa kutupilia mbali sheria hii kwa sababu kimsingi inalinda hadhi na utamaduni wetu ambao huzingatia familia kuwa taasisi muhimu kukuza jamii".

Hata hivyo, mawakili wa upande wa walalamishi wanaojumuisha hasa makundi ya jumuiya ya mapenzi ya jinsia moja maarufu kama LGBTQ wamepinga maamuzi hayo.

Wamekosoa majaji hao watano kwa kile wanachokitaja kuwa  kujenga hisia za ubaguzi wakisingizia utamaduni. Wamesema kuwa watawasilisha rufaa katika mahakama kupinga maamuzi hayo. Wakili Nicholas Opiyo na mwanaharakati Andrew Mwenda wamesema. 

Fuatilia pia: 

Museveni aitetea sheria ya kupinga ushoga

"Nadhani mahakama imekosea kwa sababu hoja iikuwa kama kuna usawa katika kulinda haki za wale tusiowapenda. Tunatumaini kukata rufaa". 

"Mahakama katika busara yake imeshinda kujitenga na dhuluma za kitamaduni na badala yake kuzingatia hisia za umma."

Angalau vipengele vinne vimeondolewa kwenye sheria hiyo na mahakama kwa ajili ya kupunguza utata kuhusiana na kuingilia masiaha ya mtu binafsi.Kwa upande wao wale wanaounga mkono sheria hiyo ikiwemo viongozi wa kidini wamefurahia maamuzi hayo.Bunge la Uganda lapitisha muswada wa sheria kali ya kupinga ushoga

Wamesema kuwa mahakama ya katiba ina jukumu la kulinda hadhi na utamaduni wa Uganda na hawatakubali mataifa ya magharibi kushinikiza kuwepo kwa mienendo ya ushoga, ulawiti na kadhalika. Uganda yapanga kutunga sheria mpya ya kupinga ushoga

 Uganda LGBTQ
Maandamano ya kupinga sheria ya LGBTQPicha: Themba Hadebe/AP/picture alliance

Wakili na mwanaharakati Gawaya Tegule amesema, "maamuzi haya ni mazuri sana na tunafurahi sana kwamba familia zetu zitakuwa na mustakabali mwema kwa sababu mahakama imetoa maamuzi yatakayowalinda watoto wetu."

Hata hivyo, watetezi wa jumuiya ya LGBTQ wameyaomba mataifa ya magharibi kutotumia sheria hiyo kuiwekea Uganda vikwazo. Yakifanya hivyo, yanajenga hisia na dhana kwamba hayaheshimu hadhi na utamaduni wa  watu wengine.