1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUganda

Uganda yapanga kutunga sheria mpya ya kupinga ushoga

1 Machi 2023

Uganda itapendekeza mswada mpya wa kupinga vitendo vya mapenzi ya jinsia moja, huku mitandao ya kijamii ikijaa uvumi kwamba kuna makundi ya kimataifa ya kukuza ushoga.

https://p.dw.com/p/4O6gZ
Kenia | LGBTQ | ugandische Flüchtlinge in Kakuma
Picha: Sally Hayden/ZUMA/imago images

Spika wa bunge Annet Anita Among hapo jana alichapisha kwenye mtandao wa Twitter video ya mkutano wa maombi alioshiriki, akisema Uganda italinda maadili na utamaduni wake kwa njia zote. Serikali za Magharibi na mashirika ya misaada yanayohudumu Uganda mara kwa mara hutuhumiwa kwa kuhimiza ushoga katika taifa hilo la Afrika Mashariki, na yamekuwa yakiitetea jamii ya watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja dhidi ya mashambulizi yanayohusishwa na mtindo wao wa kimahusiano.