1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mafuriko Afrika Kusini yasababisha vifo vya watu 22

5 Juni 2024

Mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa na upepo mkali katika pwani ya mashariki mwa Afrika Kusini yamesababisha vifo vya takribani watu 22.

https://p.dw.com/p/4gfce
Afrika Kusini mafuriko yanyesha
Jengo la ghorofa lililoharibiwa na mafuriko karibu na mji wa Durban, Afrika Kusini, Mei 23, 2022Picha: AP Photo/picture alliance

Kwa mujibu wa msemaji ya Manispaa ya Nelson Mandela Bay, watu 11 walifariki katika jimbo la Eastern Cape.Zaidi ya watu 2,000 wamehamishwa kutoka Nelson Mandela Bay, hasa wale wanaoishi kwenye mitaa ya mabanda ya manispaa hiyo.Mamlaka ya eneo hilo imetoa ombi la misaada ya nguo, chakula na mablanketi.Serikali ya mkoa jirani wa KwaZulu-Natal pia imesema watu 11 wamefariki ndani na karibu na mji wa bandari wa Durban, huku ikitangaza hali ya tahadhari katika eneo hilo. Taarifa ya serikali hiyo imesema watu 55 walipata majeraha madogomadogo hadi ya wastani na kwa sasa wanatibiwa hospitalini.