1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MADRID : Waandamana kupinga mazungumzo na ETA

4 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCVJ

Maelfu ya watu wameandamana katika mitaa ya mji mkuu wa Uhispania Madrid kupinga mazungumzo kati ya serikali na kundi la waasi la ETA wanaotaka kujitenga kwa jimbo la Basque.

Maandamano hayo yameandaliwa na chama kikuu cha upinzani cha Popular. Waandamanaji wametowa wito wa kujiuzulu kwa Waziri Mkuu wa kisoshalisti Jose Luis Rodriguez Zapatero kwa kujaribu kuwa na mazungumzo hayo kukomesha mashambulizi ya kigaidi ya kundi hilo la ETA.

Kundi la ETA lilivunja usitishaji wa mapigamo wiki tano zilizopita kwa shambulio la bomu lilotegwa kwenye gari katika uwanja wa ndege wa Madrid ambapo watu wawili kutoka Ecuador waliuwawa.

Zapatero amefuta mazungumzo hayo na ETA kutokana na shambulio hilo.