Maandamano nchini Ufaransa kuendelea | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 22.10.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Maandamano nchini Ufaransa kuendelea

Vyama sita vikuu vya wafanyakazi nchini Ufaransa vimetoa wito wa maandamano zaidi kupinga mpango wa pensheni wa serikali.

Wanawake wakishikilia bango katika maandamano.

Wanawake wakishikilia bango katika maandamano.

Paris.

Vyama sita vikuu vya wafanyakazi nchini Ufaransa vimetoa wito kwa wapinzani wa mageuzi ya mpango wa pensheni kufanya maandamano makubwa kwa muda wa siku mbili zaidi katika wiki zinazokuja licha ya kura ya mwisho kutarajiwa kupigwa na baraza la Seneti leo Ijumaa. Rais Nicolas Sarkozy , ambaye anataka kiwango cha chini cha umri wa kustaafu kiongezwe kutoka miaka 60 hadi 62 ili kupunguza gharama , amevishutumu vyama vya wafanyakazi kwa kuvuruga hatua za kufufua uchumi dhaifu wa ufaransa. Jana Alhamis polisi wa kuzuwia ghasia walipambana na vijana mjini Lyon na Poitiers wakati wafanyakazi waliogoma wakiendelea kuweka vizuwizi katika viwanda 12 vya kusafishia mafuta na robo ya vituo vya kuuzia mafuta nchini humo havina mafuta. Ni nusu tu ya treni ziendazo mikoani zimekuwa zikifanyakazi. Vyama vya wafanyakazi , ikiwa ni pamoja na chama chenye nguvu cha CGT, vimepanga maandamano Alhamis ijayo na Novemba 6. Hatua za kushughulikia maandano hayo zinazochukuliwa na rais Sarkozy zinaangaliwa kwa karibu na serikali nyingine za umoja wa Ulaya ambazo nazo zinapanga hatua za kubana matumizi.

Mwandishi : Sekione Kitojo / RTRE
 • Tarehe 22.10.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/PkbI
 • Tarehe 22.10.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/PkbI
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com