1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Liberia yapinga madai ya udanganyifu katika uchaguzi

22 Novemba 2017

Tume ya uchaguzi nchini Liberia imepinga madai ya udanganyifu yaliyowasilishwa na vyama viwili kuhusiana na matokeo ya uchaguzi wa rais yaliyopelekea mahakama ya juu kuzuia uchaguzi wa marudio uliokuwa ufanyike Novemba 7

https://p.dw.com/p/2o4Ia
Liberia Monrovia Wahlen
Picha: Getty Images/AFP/I. Sanogo

Tume ya uchaguzi nchini Liberia imepinga madai ya udanganyifu yaliyowasilishwa na vyama viwili kuhusiana na matokeo ya uchaguzi wa rais yaliyopelekea mahakama ya juu kuzuia uchaguzi wa marudio uliokuwa ufanyike Novemba 7.

Tume hiyo tayari imekuwa ikifuatilia malalamiko yaliyowasilishwa na chama tawala na chama cha upinzani cha Liberty, ambavyo wagombea wake walishika nafasi ya pili na tatu katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 10. 

Afisa wa tume hiyo, Muana Ville, amesema hajaridhishwa na malalamiko yaliyowasilishwa kutokana na walalamikaji kushindwa kuthibitisha endapo tume yake ilihusika na udanganyifu kwenye uchaguzi huo.

Vyama hivyo viwili tayari vimeitaka tume hiyo ya uchaguzi ijiuzulu. Uchaguzi wa marudio uliokuwa  ufanyike Novemba 7 uliozuiwa na mahakama ya juu nchini humo hadi pale malalamiko yaliyowasilishwa yatakapopatiwa ufumbuzi, ulikuwa umhusishe mgombea wa chama cha Unity Party, Joseph Boakai, na nyota wa zamani wa kimataifa wa kandanda, George Weah.