Lagarde kuongoza IMF
29 Juni 2011Matangazo
Bodi ya watendaji ya shirika hilo, yenye wajumbe 24, imesema jana kwamba Lagarde mwenye umri wa miaka 55, ataanza kutumikia awamu ya kwanza ya miaka mitano, kuanzia Julai 5.
Bibi Lagarde amechukua nafasi ya Mkurugenzi mtendaji wa zamani Dominique Strauss Kahn, ambaye alijiuzulu mwezi Mei, kutokana na tuhuma za kumbaka mhudumu mmoja wa hoteli, mjini New York, Marekani.