1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIndonesia

Kura zaendelea kuhesabiwa nchini Indonesia

Zainab Aziz
14 Februari 2024

Mamlaka za uchaguzi nchini Indonesia zinaendelea na zoezi la kuhesabu kura baada ya kufanyika uchaguzi wa rais nchini humo ambapo mshindi atachukua nafasi ya rais Joko Widodo

https://p.dw.com/p/4cO3X
Indonesien Timika | karatasi ya kura
Karatasi ya kuchagua Rais IndonesiaPicha: Adek Berry/AFP/Getty Images

Kinyanganyiro hicho ni kati ya magavana mawili,  Ganjar Pranowo na Anies Baswedan, wanaoshindana na mjumbe mwingine mtatanishi ambaye ni waziri wa ulinzi Prabowo Subianto.

Matokeo yanatarajiwa kuanza kutolewa baadaye leo.  

Soma pia:Prabowo wa Indonesia ajitapa kuwa atashinda urais wiki ijayo

Matokeo ya uchaguzi yatakuwa na umuhimu hadi nje ya mipaka ya Indonesia ambapo mshindi atapaswa kujipanga ili kukabiliana na ushindani, unaoongezeka kati ya China na Marekani.